
Mbunge mteule wa jimbo ya Muhambwe, Dk. Florence Samizi (CCM) akikabidhiwa hati ya ushindi na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Diocles Rutema
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimefanikiwa kutetea majimbo ya Buhigwe na Muhambwe mkoani Kigoma, baada ya kushinda kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika jana Jumapili, tarehe 16 Mei 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).
Katika uchaguzi huo, CCM kilichuana vikali na ACT-Wazalendo, ambapo waliogombea Jimbo la Muhambwe ni, Dk. Florence Samizi (CCM) na Julius Masabo (ACT-Wazalendo) na Buhigwe, Galula Kudra (ACT-Wazalendo) na Mwalimu Eliadory Kavejuru (CCM) .
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo jana usiku, Msimamizi wa Uchaguzi Muhambwe, Diocles Rutema, amesema, Dk. Samizi ameshinda baada ya kupata kura 23,441, huku aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Masabo akipata 10,847.

Wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na aliyekuwa Mgombea wa Democratic Party (DP), Philipo Fumbo aliyepata kura 368.
Kwa upande wa Buhigwe, Msimamizi wa uchaguzi huo, Marycelina Mbehoma, amesema Dk. Kavejuru ameshinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 25,274 kati ya kura 30320 halali zilizopigwa.
Chaguzi hizo ziliitishwa na Tume ya Taufa ya Uchaguzi (NEC), baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo kuachwa wazi, kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe (CCM), Atashasta Nditiye, kufariki dunia na Dk Phillip Mpango, aliyekuwa Mbunge wa Buhigwe (CCM), kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais na Rais Samia Suluhu Hassan.
More Stories
Shaka atembelea MwanaHALISI, Raia Mwema
Shule za Serikali, wasichana wang’ara matokeo kidato cha sita
Jamhuri yakwamisha kesi ya Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi