CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimetangaza kamati yake ya kampeni itakayofanya kazi ya kukitafutia ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Kamati hiyo yenye majina 32 itaongozwa na Abdulrahiman Kinana, Rajab Luhwavi, Makamu Mwenyekiti Bara na Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti Zanzibar. Anaandika Pendo Omary …(endelea).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kwa vyombo vya habari inasema “uteuzi wa majina 32 ya kamati hiyo ulitokana na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika jana katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.”
Pia, kikao hicho kilikamilisha uteuzi wa wagombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika majimbo ya Singida Mashariki ambapo ameteuliwa Jonathan Njau na Kiteto ambapo ameteuliwa Emmanuel Paplam.
KAMATI YA KAMPENI YA CCM
- Abdulrahiman Kinana – Mwenyekiti
- Rajab Luhwavi – Makamu Mwenyekiti Bara
- Vuai Ali Vuai – Makamu Mwenyekiti Zanzibar
- Sofia Simba
- Mohamed Seif Khatib
- Asha – Rose Migiro
- Samuel Sitta
- Nape Nnauye
- Mwigulu Nchemba
- Harrison Mwakyembe
- January Makamba
- Amina Makillagi
- Chrstopher Ole Sendeka
- Stephen Wasira
- Abdallah Bulembo
- Hadija Aboud
- Mohamed Aboud
- Lazaro Nyarandu
- Issa Haji Ussi
- Waride Bakari Jabu
- Mahmoud Thabit Kombo
- Shamsi Vuai Nahodha
- Maua Daftari
- Stephen Masele
- Pindi Chana
- Shaka Shaka
- Makongoro Nyerere
- Bernard Membe
- Sadifa Juma Khamis
- Antony Diallo
- Livingstone Lusinde
- Ummy Mwalimu
More Stories
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani
Kuvunjwa kwa Jiji la Dar giza nene latanda
Ukomo wa urais uheshimiwe