January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM yapuuza msiba wa Dk. Makaidi

Spread the love

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepuuza kushiriki katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Nation Legue For Demokracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi kwenye Ukumbi wa Karem jee leo Jijini Dar es Salaam. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Awali mwili wa Makaidi ambaye pia alikuwa mwenyekiti mwenza wa vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ulifikishwa ukumbini hapo saa 5:45 asubuhi ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo wa kisiasa wakishiriki.

Viongozi waliohudhulia katika shughuli hiyo ni pamoja na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa; Mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe; Mgombea Mwenza wa Chadema, Babu Duni; Mke wa Lowassa, Regina Lowassa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Francis Mbatia.

Viongozi wengine wa vyama ni mshauri wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu; Waziri Mkuu Mstaafu, Fredirick Sumaye; Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kawe, Halima Mdee; Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea pia Mgombea Urais wa Chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa.

Wengine ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi, mwakilishi kutoka Jukwaa la Wahariri (TFF) pamoja na Simba Sport Klabu.

Waliotoa salamu za rambirambi kwenye shughuli hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa NLD, Mfaume Hamisi, Baregu mwakilishi wa Maveteran, Jaji Mutungi, Peter Mzirai kwa niaba ya Baraza la Vyama vya Siasa (TCD) pamoja na mwakilishi wa familia ambapo pamoja na CCM kuwepo kwenye ratiba ya kutoa salamu, hakuwepo mwakilishi kutoka chama hicho.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula aliibuka dakika 10 kabla ya mwili wa Makaidi kuondolewa viwanjani hapo.

Waandishi walipotaka kujua sababu ya kuchelewa kwake kwenye shughuli hiyo, Mangula aligoma kuzungumzia suala hilo ambapo alibaki kuwa mtazamaji wa shughuli ya kuondoa mwili wa makaidi viwanjani hapo.

Mwili wa Makaidi uliondoka katika ukumbi huo saa 8:40 mchana na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya Sinza saa 11 jioni.

error: Content is protected !!