July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM yapukutika Arusha

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole (katikati). Kushoto ni Katibu Mwenezi wa mkoa, Isaac joseph (Kadogoo).

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kupata pigo kwa kuondokewa na wanachama wake. Mara hii, Onesmo Nangole na Isaac Joseph, wametangaza rasmi kukihama chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Nangole, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, mkoani Arusha na Isaac aliyekuwa katibu mwenezi wa mkoa huo, wametangaza rasmi kuachana na CCM na kuhamia Chadema, mchana huu mbele ya waandishi wa habari.

Alisema, “…CCM kimekosa misingi yake ya asili iliyokiunda. Imeacha kusimamia haki na usawa,” na kuongeza, “hivi sasa chama hiki, kimekuwa gulio la wahalifu na chama cha watu wachache ambao wamekuwa wakichuka maamuzi kwa faida yao binafsi.

Naye Isaac, maarufu kama Kadogoo amesema, kudhihirisha kuwa CCM sasa inaendeshwa kwa maslahi ya watu wachache; mchakato wa kumpata mgombea wake urais, uligubikwa na mizengwe na kusema kuwa kama kanuni na taribu zingefuatwa, Edward Lowasa ndiye angechaguliwa katika mchakato ule.

Mwenyekit wa Chadema wilaya ya Arusha, Magoma Derick Magoma amesema chama hicho kinawakaribisha wote wanaoijisika kuunga nao katika harakati za mabadiliko.

Nangole ambaye amekitumikia CCM toka mwaka 1977 anakuwa mwenyekiti wa pili wa mkoa kukihama chama hicho.

Wiki iliyopita, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai na ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM Taifa,  alihamia Chadema siku chache zilizopita.

error: Content is protected !!