CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza safu mpya уа Wajumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC), baada ya vikao vya Kamati Kuu na NEC vilivyofanyika, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, tarehe 14 Januari, 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika safu hiyo, iliyotangazwa na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka baada ya vikao hivyo, safu hiyo inajumuisha wajumbe saba kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.
Wajumbe hao wa Kamati Kuu (CC) kutoka Tanzania Bara ni; Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mstaafu Hassani Wakasubi na Katibu wa zamani wa UWT Halima Mamuya.
Kutoka Zanzibar Wajumbe wa Kamati Kuu hiyo ni Mohammed Aboud Mohamed, Mhandisi Nassir Ali Juma na Laila Burhan Ngozi.
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Sekretarieti ni; Katibu Mkuu – Daniel Chongolo (wa awali), Naibu Katibu Mkuu Bara- Anamringi Macha (mpya), Naibu Katibu Mkuu Zanzibar – Mohamed Said Mohamed
‘Dimwa’ (mруа) na Katibu wa NEC Idara ya Itikadi na Uenezi – Sophia Mjema (mpya).
Wengine ni Katibu wa NEC Idara ya Uchumi na Fedha – Dk. Frank Hawasi (wa awali), Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) – Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mpya) na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni – Issa Ussi.
Leave a comment