January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM yaonya gazeti lake Uhuru kisa uchaguzi 2025

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM

Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitachukua hatua kali dhidi ya watumishi wa gazeti la Uhuru kwa kuandika habari ya upotoshaji juu ya Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya gazeti hilo linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Jumatano tarehe 11 Agosti 2021, kuandika habari kuwa Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, hana mpango wa kuwania urais mwaka 2025.

Chanzo cha habari hiyo, imeelezwa na gazeti hilo ni mahojiano ambayo Rais Samia aliyafanya hivi karibuni na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Hata hivyo, taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka, imesema habari ya gazeti la Uhuru yenye kichwa cha habari cha ‘Sina wazo kuwania urais 2021-Samia’ ni ya upotoshaji.

“CCM kimesikitishwa na upotoshaji mkubwa uliofanywa na Gazeti la Uhuru toleo Namba 24084, la leo Jumatano tarehe 11 Agosti 2021. Gazeti hilo limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais Samia na BBC, Ikulu Dar es Salaam,” imesema taarifa ya Shaka.

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Katika taarifa yake, Shaka amesema habari hiyo iliyoandikwa na Gazeti la Uhuru ni ya upotoshwaji mkubwa, kwani katika mahojiano hayo, Rais Samia hakusema maneno hayo.

“Katika habari yake kuu limeandika kichwa cha habari ‘Sina wazo kuwania urais 2025-2025’. Huu ni upotoshwaji mkubwa na kumlisha maneno Rais wa Tanzania, hakusema kabisa maneno hayo,” imesema taarifa ya Shaka.

Shaka amesema CCM itachukua hatua za kinidhamu dhidi ya watu waliohusika na uandaaji wa habari hiyo.

“Hili ni kosa kubwa linalokwenda kinyume ana sera inayoongoza vyombo hivyo, jambo ambalo halitavumiliwa hata kidogo, hivyo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote waliohuisika katika uandaaji wake,” imesema taarifa hiyo.

“Gazeti la Uhuru ndiyo Adam na Hawa wa magazeti yote hapa nchini, Linawajibika kunesha weledi wa hali ya juu na sio vinginevyo.”

“Tunawoamba wanachama wa CCM na Watanzania kwa ujumla kupuuza habari hiyo kwani iemandikwa na watu wenye maslahi yao binafsi,” amesema

Shaka amesema, Rais Samia kwa sasa ameelekeza fikra na nguvu zake katika kuwatumikia Watanzania na si vinginevyo.

error: Content is protected !!