Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yaongeza wajumbe NEC kutoka 15-20
Habari za SiasaTangulizi

CCM yaongeza wajumbe NEC kutoka 15-20

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

NAFASI za idadi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), imeongezwa kutoka wajumbe 15 hadi 20 Tanzania Bara vivyo hivyo kwa upande wa Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Aidha, nafasi za uteuzi kwa wajumbe wa NEC zinaongezeka kutoka sita hadi 10 wakati nafasi ya ukatibu wa siasa na uenezi wa mikoa zitakuwa ajira badala ya nafasi za kuteuliwa.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 7 Disemba, 2022 na Wajumbe wa Mkutano mkuu waliopitisha marekebisho ya Katiba ya chama hicho yaliyopendejezwa na Katibu Mkuu Daniel Chongolo.

Hatua hiyo imekuja baada Rais Samja Suluhu Hassan kuwahoji wajumbe hao katika mkutano mkuu wa 10 wa CCM unaondelea Jijini Dodoma.

Awali Dk. Samia ametaja sababu mbalimbali za mabadiliko hayo ya katiba hasa nafasi ya uenezi ndani ya CCM kuwa ya kuajiriwa kwamba aina ya waliokuwa wakichaguliwa walishughulika na kuimba katika mikutano badala ya kueneza siasa ya CCM.

Amesemq inawezekana kuna sababu nyingi mathalani uwezo na ili chama kisemewe vizuri kuanzia ngazi ya mkoa nafasi ya uenezi iwe ya ajira.

“Hatua hii itafanya awajibike vizuri kukisemea chama, kwa sababu ni nafasi ya ajira itakuwa ina vipimo kwamba unafanya vizuri utaendelea au unafanya vibaya mkataba utasitishwa ili awekwe mwingine atakayekuwa na sifa ya kukisemea chama.

“CCM imeamua katika ngazi ya mikoa makatibu wenezi wapatikane kwa mfumo wa ajira,” amesema.

Amesema wenezi walioko katika mikoa wameongezewa muda hadi miezi mitatu kutumikia nafasi hiyo wakati mchakato wa kuwapata wengine ukiendelea.

“Kilikuwa kilio kikubwa, kwamba hawaingii, hawatumiki na wanajiona hawashirikishwi, sasa tumeamua wapangaiwe majukumu maalumu,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!