Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshangazwa na ukimya kwa wakuu wa mikoa (RC) na wilaya (DC) katika kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Hayo yamesemwa jana Jumamosi, tarehe 14 Mei 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho Mjini Babati Mkoa wa Manyara.

Shaka alisema hayo katika mkutano wa ndani wa kujitambulisha mbele ya wanachama wa CCM kama mlezi mpya wa chama hicho akichukua nafasi ya Waziri mkuu mstaafu, Mzee Mizengo Pinda.

“Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya kote nchini mna jukumu la kuyaeleza mafaniko ya serikali ya Mama Samia…sasa hivi kuko kimya hamumtendei haki Rais wetu,” alisema.

Shaka alisema katika utafiti aliyofanya miaka miwili iliyopita kila mkuu wa mkoa na wilaya walikuwa wakitoa taarifa za mafanikio ya serikali kinyume na hali ilivyo sasa.

Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wake Rais Samia amefanya makubwa kana kwamba amekaa miaka mitano yakiwemo kuifungua Tanzania kiuchumi na kidiplomasia.

“Rais Samia ni kinara wa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, hilo liko wazi, lazima tuyaseme mafanikio hayo,” alisema Shaka kwa ukali.

Rais Samia toka aingie madarakani amechukua hatua kadhaa za kulainisha uhasama na kuponya vidonda

2 Responses

  1. Asante ndugu shaka nategemea wakuu wa wilaya and wakuul.wamikoa wamekusukia na maelezo yako shaka ni yaukweli sasa hata upangaji biashara katika njia ya watembea kwa miguu umerudi tena mkuu wa wilaya mkuu wa mkoa hata habari hawana maana yake tutajijua wenye

  2. Duh!
    Shaka, umeikosea mbinu ya mama.
    Anatumia kalamu. Hataki kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
    Alisema wananchi wabebe mabango… mbona wewe unataka arejeshe lile gari bovu. Wewe upo kwenye Chama, kahamasishe wananchi!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *