CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa wasiwasi Rais Samia Suluhu Hassan, kuhusu mikutano ya hadhara kwa kusema kuwa itatumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi mazuri yaliyofanywa na Serikali yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 10 Januari 2023 na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, akizungumza katika hafla ya kufunga matembezi ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Visiwani Zanzibar, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia.
Katibu Mkuu huyo wa CCM amempongeza Rais Samia kwa uamuzi wake wa kuondoa zuio la mikutano hiyo akisema itakisaidia chama chake.
“CCM kimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama, kwetu sisi CCM hiyo ni fursa muhimu na kubwa kwani tunakwenda kuitumia kueleza umma kile ambacho Serikali zetu zinafanya katika kutekeleza ilani ya chama. Nikuhakikishie hiyo fursa usiwe na wasiwasi nayo tuko makamanda wako,” amesema Chongolo na kuongeza:
“Tuko wasaidizi wako ambao tuko tyimamu tunakuhakikishia tutaitumia ipasavyo kuhakikisha tunapeleka kwa umma kile ambacho tunakifanya kupitia serikali zetu.”
Leave a comment