Monday , 29 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yamtamani Katibu Chadema
Habari za Siasa

CCM yamtamani Katibu Chadema

Spread the love

KATIBU Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wilayani Bahi jijini Dodoma, Melickzedeck Lesaka ametoa siku saba kwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bahi kumuomba radhi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Ametaka kuombwa radhi kwa madai kuwa, UVCCM wamekuwa wakipotosha umma kuwa, amehamia chama tawala (CCM).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 15 Julai 2019 Lesaka amesema, ameamua kuweka wazi msimamo wake kwamba, hajahamia CCM na kwamba, baada ya kustaafu siasa, anafanya kazi ya injili.

“Nimesikitishwa sana na kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM, Hasani Kadoki kufanya mkutano na kuutangazia umma kuwa, mimi Lesaka nimejiunga CCM kwa kuunga juhudi za serikali. Siyo kweli.

“Kibaya zaidi, habari hizo zimesambaa katika baadhi ya vyombo vya habari, jambo ambalo limenisababishia usumbufu mkubwa kwa jamii kwamba nimewasaliti watu ambao wananiamini katika utendaji kazi wangu,” amesema.

Lesaka amesema kuwa, aliwaaga wananchi kuachana na siasa na kwenda kwenye masomo. “Mimi nilifanya mkutano na kuwaaga wananchi kuwa, nakwenda masomoni na sitakuwa katika mikakati ya kisiasa kwa muda bali nitakuwa katika huduma ya injili.”

Amesema, hajawahi kuhudhuria mkutano wowote wa UVCCM na hajachukua kadi ya chama hicho “sijawahi kuchukua kadi ya CCM, mimi siyo mwanachama wa CCM na wala sijawahi kupeleka kadi yangu ya Chadema kwao CCM.

“Kitendo cha kutangaza kuwa nimehamia CCM, ni kunidhalilisha na kunisababishia usumbufu sambamba na kuifanya jamii kutoniamini.”

Hasani Kadoki, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bahi amekiri kuwa, hawajawahi kumpokea Lesaka wala kupokea kadi yake ya Chadema au kumpa kadi ya CCM.

Amesema kuwa, alilazimika kumtangaza hadharani katika mkutano wa CCM kutokana na kupokea taarifa zake za kuhama kutoka kwa Mchungaji Damiani ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Chikola, Wilaya ya Bahi.

“Baada ya kufika Kata ya Chikola nikiwa mgeni rasmi nikiwa nawapokea baadhi ya wanachana wa Chadema na kujiunga CCM, ndipo Mchungaji alisema kuwa, Lesaka ametoa salamu na kueleza kuwa yupo pamoja na CCM, na yeye yupo mbioni kujiunga na CCM,” ameeleza Kadoki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!