WANACHAMA watatu wa Chama cha ACT -Wazalendo akiwemo aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro kusini Mashariki mwaka 2015 na Mwenyekiti wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Christina Haule.
Wanachama hao yumo aliyekuwa mgombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita Dk. Daud Mollel, Mwenyekiti wa chama hicho Dk. Hamimu Hongo na Yahya Nasoro mwanachama wa kawaida ambao wameamua kujiunga na CCM.
Wanachama hao wamesema kwa sasa hawana sababu ya kuendelea kubaki upinzani kutokana na utendaji wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.
Chama hicho ambacho kimepata pigo kinaoongozwa na Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini.
Makada hao wapya wa CCM walijitokeza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoani morogoro na kuweka bayana dhamira yao ya kuhamia CCM na namna walivyoguswa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge ameitaka jamii kuendelea kuwa na imani na serikali pamoja na kuendeleza ushirikiano katika kutekeleza Ilani ya chama ambayo ndiyo mwongozo kwa serikali.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro, Fikiri Juma amewataka wanasiasa hususani wa vyama vya upinzani kuangalia namna ya kushirikiana na serikali katika kupigania rasilimali za nchi na kuachana na siasa zisizo zingatia uzalendo.
Leave a comment