Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yalia miradi ya maendeleo kukwama, yatoa siku 14
Habari za Siasa

CCM yalia miradi ya maendeleo kukwama, yatoa siku 14

Spread the love

 

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimezipa siku 14 kamati za siasa za mikoa na wilaya, kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kwenye Sekretarieti ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo Jumanne, tarehe 10 Agosti 2021 na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, katika ziara yake mkoani Morogoro.

“Tunatoa siku 14, sisi sekretarieti tupokee taarifa kutoka mikoa yote ya kile mnachokiona huko katika kukagua miradi, ili tutoe malekezo ya kuweka msukumo penye kuwekwa msukumo, kurekebisha mambo ambayo tunaona hayaendi,” amesema Chongolo.

Katibu Mkuu huyo wa CCM, ametoa agizo hilo baada ya kubaini kwamba kuna baadhi ya miradi ya maendeleo, imekwama kwa sababu mbalimbali.

“Nina taarifa kuna mardi bado haijamalizwa , haya maelekezo na maagizo naiwajibu wa ngazi zote kutekeleza. Wale ambao bado, tunawapa siku 14 wakamilishe hilo zoezi. Hili jambo ni la wajibu na lazima,halina hiyari,” amesema Chongolo.

Aidha, Chongolo amewaagiza viongozi wa CCM wa mikoa, wilaya hadi ngazi za chini, kuweka mikakati ya kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya 2020-2025.

“Natoa maelekezo na nitatoa agizo kwamba tutamaliza mkutano mkuu maalum, sasa kazi iliyopo ni kwa timu zote kwenda chini kuweka mfumo wa kukagua miradi au utekelezaji ilani,” amesema Chongolo.

Mwanasiasa huiyo amesema kuwa, kitendo cha miradi hiyo kutokamilishwa kwa wakati au kutotekelezwa kabisa, kunawafanya waonekane waongo mbele ya wananchi.

“Sababu kuna miradi inasimama, wanaotakiwa kutoa hela hawatoi hela, sisi ndiyo tunaokuja kuulizwa mwishoni kwamba fedha hazijashuka, miradi haijatekelezwa. Ni aibu, sisi hatuko tayari kuonekana waongo,” amesema Chongolo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!