Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yalia kuibiwa kura
Habari za Siasa

CCM yalia kuibiwa kura

Spread the love

ZAIDI ya wanachama 1,100 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mwakizega, Uvinza mkoani Kigoma, wamerejesha kadi za chama hicho wakidai, mgombea wa chama cha DP aliiba kura za mgombea wao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Wanachama hao wamewatuhumu viongozi wa kata hiyo kubariki rafu zilizofanywa na Patrick Bitaliho, mgombea wa DP na kusababisha mgombea wao Swabiru Mussa, kushindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 Oktoba 2020. Kwenye kata hiyo Bitaliho alitangazwa mshindi.

Wanachama hao wameeleza, kwamba walikutana na viongozi wa chama katika kata yao na kuwataka wafuatilie hujuma hizo, lakini mpaka wanachukua uamuzi huo, hakuna hatua zozote zilizokuwa zimechukuliwa.

“Hatua ya mgombea wetu kufanyiwa mziengwe ili aangushwe imetuumiza wengi, viongozi nao hakufuatilia licha ya kuwapa taarifa hiyo,” amesema Hafsa Ramadhani, mwachama wa chama hicho aliyedai kurejesha kadi yake.

Juma Yassin amesema, amuamua kurejesha kadi yake ya uanachama kwa Katibu wa CCM wa Kata ili kuonesha namna alivyokasirishwa na hujuma, pia uzembe wa viongozi wa kata kufuatilia madai yao.

Mbano Gwemela, Katibu wa CCM Kata ya Mwakizega amesema, amepokea kadi zaidi ya 1,100 za waliokuwa wanachama wa chama chake kwa madai ya kukasirishwa na hujuma zilizofanyika kwenye uchaguzi mkuu.

“Hapa nilipo kuna kadi 360 kutoka Kijiji cha Katete na kadi 740 zinatoka katika Kijiji cha Mwakizega. Kwa kweli jambo hili linanipa wakati mgumu sana kukabiliana nalo na wanachama hawataki kuelewa lolote kwa sababu bado wana hasira,” alisema Gwemela.

Mgombea mwenyewe Swabiru amedai, aliibiwa kura zake na Bitaliho wa Chama cha DP na kwamba, amepanga kukata rufaa. Madai hayo yameelezwa kwamba baadhi ya vituo taa zilizimwa kwa makusudi, vituo vingine matokeo yalibadilishwa na kumpa ushindi mgombea wa DP.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!