MATOKEO ya Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania uliofanyika Jumatano iliyopita tarehe 28 Oktoba 2020 yanaonyesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejikusanyia viti vingi vya udiwani na ubunge. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Hadi kufikia saa 7 mchana, matokeo hayo yanayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yanaonyesha CCM imekwisha kujikusanyia majimbo 220 kati ya 264.
Chadema ina mbunge mmoja, Aida Khenan wa Nkasi Kaskazini ambaye amemuangusha mbunge wa CCM aliyekuwa anaongoza jimbo hilo kwa miaka kumi mfululizo Ally Kessy.
Aida Khenan
Jimbo jingine ambalo upinzani wamejikusanyia ni la Mtwara Vijijini ambalo Shamsia Mtamba wa CUF amemuangusha mbunge wa CCM aliyekuwa anatetea jimbo hilo, Hawa Ghasia.
Shamsia Mtamba
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2015, kati ya majimbo 264, upinzani walijikusanyia majimbo zaidi ya 65 lakini mpaka sasa, majimbo yaliyosalia kutangazwa ni 45 pekee.
Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali.
Leave a comment