Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yajihami kimataifa
Habari za SiasaTangulizi

CCM yajihami kimataifa

Rais John Magufuli akiongoza Kamati Kuu ya CCM
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimezitaka Jumuiya za Kimataifa kupuuza malalamiko ya vyama vya wapinzani nchini, kwamba vinahujumiwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari tarehe 13 Novemba 2019, jijini Dar es Salaam, Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema, madai ya wapinzani si ya kweli, na kwamba vyama hivyo havikufuata utaratibu na sheria za uchaguzi.

“Wenzetu sasa hivi wanakusanya habari za kuunga wapeleke kwa nchi za ng’ambo, sisi tunakusanya taarifa tunawapeleka Watanzania. Sijui dhamira yao ni ipi? 

“Lakini haki tumeitenda kama taifa na sisi tumeridhika kama chama, kwamba mchakato wa uchaguzi ulikuwa wa haki, umeonewa kata rufaa,” ameeleza Polepole.

Amedai, vyama vya siasa vya upinzani vilivyojitoa kwenye uchaguzi huo, vimekosa itikadi na sera za kuwaeleza Watanzania, na kwamba wamebakiwa na midomo tu, wanayoitumia kuongea pasipokuwa na hoja za msingi, na kuwa suala hilo halivumiliki popote ulimwenguni.

“Vyama vya siasa ambavyo vimekosa itikadi, havina msingi, havina masuala ya kuwaonesha watu, wamebakiwa na midomo na wanahubiri bila ya kuwa na itikadi, hiki hakiwezi kuvumiliwa mahali popote na raia wanaonesha uvumilivu wao katika sanduku la kula,” amesema Polepole.

Polepole amezieleza Jumuiya za Kimataifa kuwa, Tanzania ni nchi huru, inayoheshimu na kutekeleza sheria na mikataba ya kimataifa, kuhusu kulinda haki za binadamu.

“Tanznaia ni nchi huru inayozingatia sheria za kimataifa na misingi ya haki za binadamu, hapa Tanzania watu wako huru kueleza maoni na mawazo yao, ahadi nyingi tulizoahidi mwaka 2015 tumezitekeleza kwa kiwango kikubwa kuwahi kushuhudiwa,” amesema Polepole.

Polepole amewakaribisha raia wa mataifa wa nje, kuja kushuhudia namna Tanzania inavyoleta maendeleo kwa watu wake.

Hata hivyo, Polepole amesema CCM inaitaka serikali yake iendelee kuchapa kazi kwa kuwa, imewekwa madarakani na Wananchi wa Tanzania, na si raia wa mataifa ya nje.

Polepole anazungumza hayo wakati vyama vya upinzani nchini, vikiendelea na msimamo wa kutoshiriki uchaguzi huo kwa madai ya kuchafuliwa na wasimamizi wake.

Baadhi ya vyama, vinaishutumu CCM na serikali yake, kucuruga uchaguzi huo kwa maslahi ya chama tawala (CCM).

Vyama ambayo vimejitenga na uchaguzi huo ni pamoja na Chadema, ACT-Wazalendo, CUF, UPDP, NCCR-Mageuzi, Chaumma, NLD na CCK.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!