April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CCM yahamia Mwanza, kuvuruga upinzani

Rais John Magufuli akiongoza Kamati Kuu ya CCM

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepanga kufanyia mikutano yake ya Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) na Kamati Kuu (CC), mjini Mwanza, kuanzia wiki hii. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mbali na mikutano hiyo, chama hicho, kinakusudia kufanyia semina wajumbe wa NEC.

Mtoa taarifa wa MwanaHALISI ameeleza kuwa mikutano yote hiyo, itafanyika mara baada ya kumalizika sherehe za uhuru, zinazoendelea mjini humo.

“Tutahamia Mwanza, kujiimarisha kisiasa. Tumepanga kufanya mikutano yetu ya Kamati Kuu na NEC mjini humo, ili kujihakikishia kuwa eneo hilo la Kanda ya Ziwa Victoria, bado linabaki kuwa ngome yetu,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa chama hicho.

error: Content is protected !!