Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yafunga pazia fomu kuwania uspika, 69 warejesha
Habari za Siasa

CCM yafunga pazia fomu kuwania uspika, 69 warejesha

Spread the love

DIRISHA la kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa katika nafasi ya uspika kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 15 Januari limefungwa rasmi saa 10 kamili jioni. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma… (endelea)

Katika zoezi la uchukuaji fomu, jumla ya wanachama 71 wa CCM wamechukua fomu ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge iliyoachwa wazi baada ya Job Ndugai kujiuzulu tarehe 6 Januari mwaka huu huku wanachama wawili kushindwa kurejesha fomu.

Uchukuaji wa fomu hiyo umewakusanya makada mbalimbali wakiwemo, mawakili, waliowahi kuwa wabunge na mawaziri, aliyewahi kuwa katibu wa Bunge, aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali na vigogo mbalimbali ndani ya serikali na ndani ya siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 15 Januari,2022 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganazesheni CCM, Solomon Itunda amesema idadi ya wanachama waliochukua fomu katika siku ya mwisho wa zoezi hilo imefika 71.

Amesema kwa siku ya leo jumla ya wanachama watano walichukua fomu na kufanya idadi kufikia wanachama 71 baada ya wale 66, waliokuwa wamechukua hadi juzi.

“Leo tumepokea wanachama watano ambao wamejitokeza katika vituo vyetu vya Dodoma na Dar es saalam kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hii ya Uspika iliyoachwa wazi.

Aidha, amesema katika kituo cha Dodoma mwanachama mmoja ndiye aliyejitokeza kuchukua fomu wakati katika ofisi ya Lumumba ni wanachama wanne na afisi kuu ya Zanzibari hakuna aliyechukua.

Itunda, alimtaja aliyechukua fomu ofisi kuu Dodoma kuwa ni Samwel Magero.

“Ofisi ndogo ya Lumumba waliochukua fomu ni Rahimuddin Ismail, Alex Mwita,Themistocles Laurian Rwegasira pamoja na Grangay Nyalohala” amesema.

Amesema kukamilika kwa zoezi hilo la kuchukua fomu lililoanza tarehe 10 Januari, mwaka huu, kunatoa nafasi kwa vikao vingine kuanza.

“Baada ya zoezi hili la kuchua na kurejesha fomu sasa hatua inayofuata ni vikao vingine kuketi ili kuanza kufanya mchujo wa kupitisha jina moja litakalokiwakilisha chama katika kugombania nafasi hii ya Uspika”amesema.

Amesema pamoja na wanachama hao 71 kuchukua fomu lakini kati yao wawili wameshindwa kurejesha.

Aidha, ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha demokrasia ndani ya chama hicho.

“Lakini pia ninawashukuru wanachama wote ambao wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama”alisema Itunda

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!