Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yaeleza mageuzi iliyofanya kwenye elimu tangu uhuru
Habari za Siasa

CCM yaeleza mageuzi iliyofanya kwenye elimu tangu uhuru

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema tangu kimechukua madaraka baada ya Tanzania kupata uhuru, kimefanya mageuzi mengi katika sekta ya elimu, kwa kujenga vyuo vikuu, vya kati na shule za sekondari na msingi nchi nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 1 Machi 2023 na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa, katika mageuzi kwenye sekta ya elimu, Serikali zilizoongozwa na CCM zimefanikiwa kujenga vyuo nchi nzima, tofauti na ilivyokuwa kabla ya uhuru ambapo hakukuwa na chuo hata kimoja.

“Leo CCM kama tungekuwa wabaguzi tungesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ni cha CCM sababu tulikianzisha wenyewe. Lakini hatukuanzisha kwa ajili ya CCM, lakini kilianzishwa kwa ajili ya Watanzania na kwa sababu CCM inaangalia mambo kwa ajili ya Watanzania na sio kwa ajili yake ndiyo maana likatengwa eneo la kutosha,” amesema Chongolo.

Mbali na ujenzi wa vyuo vikuu na kati nchini, Chongolo alisema mageuzi mengine yaliyofanyika kwenye sekta ya elimu ni kujenga shule za sekondari na msingi, pamoja na kusambaza walimu nchi nzima.

“Mapinduzi ya elimu yameenda hatua kwa hatua, 1977 tulikuwa na changamoto kubwa tulikuwa na shule nyingi hatuna walimu. Mwishoni mwa 1970 Serikali ilifanya uamuzi ikachukua wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakapelekwa kufanya mafunzo kwa muda mfupi wakaitwa walimu wa UPE na walikuwa bora,” amesema Chongolo na kuongeza:

“2003 tukafanya maamuzi ya kuanzisha shule kwenye kata, 2004 tukajenga kisha 2007 tukafanya uamuzi wa kuanzisha utaratibu wa walimu wanapewa leseni wanaenda kufundisha wakaitwa voda fasta leo wanafunzi wake wanapata daraja la kwanza. Mipango haizaliwi kwa ndoto, huzaliwa kwa watu kukaa chini na kutafuta njia ya kutatua changamoto.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!