January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM `yabomoka` Diwani, wanachama 100 wajiunga CUF

Mwenyekiti wa sasa wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo

Spread the love

HALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza si shwali baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo (Fashion), na wanachama zaidi ya 100 kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF). Anaandik Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwendelezo wa wimbi la wanachama wa CCM kuhamia upinzani hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA.

Diwani na wanachama hao kutoka matawi mbalimbali ya CCM, walieleza chanzo na sababu za kutimkia CUF, kuwa chama hicho kimetawaliwa na vitendo vya rushwa, chuki na undugu kitendo kinachosababisha kukosekana kwa demokrasia ya kweli.

Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia rushwa kushika madaraka na kusababisha watu ambao ni wazalendo wenye nia dhabiti ya kuwatumikia wananchi kukosa haki hiyo.

Wanachama hao wakiongozwa na diwani huyo, walipokelewa leo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Karume Jeremiah, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Chakechake, Nyamagana.

Akizungumzia tamko la wao kujiengua CCM na kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo alivyodai vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu na hila na kukosekana kwa demokrasia.

“Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magori ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa tumekuja huku upinzani. Lazima tuwashughulikea mpaka waachane na wizi wao.

“Niliwania udiwani kwa mara nyingine tena, hila na tamaa ya CCM walinikata jina kwa sababu nilikuwa napingana nao, walipolazimisha fedha za miradi ya wananchi tuzitumie kwa mambo ya chama,” amesema Fashion.

Kwa upande wake, Jeremiah amesema kutokana na CCM kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo, sasa umefika wakati wakaipisha UKAWA kuingia `magogoni` ili kutatua kero za watanzania.

error: Content is protected !!