June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM yabariki “kitanzi” cha vyombo vya habari

Jengo la Bunge la Tanzania

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimearifiwa rasmi na Serikali yake kwamba inawasilisha bungeni miswada miwili ya habari ya mwaka 2015, chini ya hati ya dharura Ijumaa wiki hii kwa lengo la “kuvibana” baadhi ya vyombo vya habari. Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo wadau wa habari wamepiga kambi mjini Dodoma tangu Jumamosi iliyopita na kumwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda wakimwomba atumie hekima kuishauri serikali isiwasilishe miswada hiyo ya Haki ya Kupata Taarifa na ule wa Huduma za Vyombo vya Habari chini ya hati ya dharura.

MwanaHALISIOnline limeona waraka wa mawasiliano baina ya viongozi waandamizi wa CCM, ambapo Baraza Kuu la Taifa la Umoja wa Wazazi lililokuta Dodoma liliarifiwa kuhusu lengo la serikali.

Waraka huo unasema, “Nilikuwa kwenye kikako cha kawaida cha Baraza Kuu la Taifa la Umoja wa Wazazi kilichofanyika kwa siku moja mjini Dodoma, Jumamosi kisha kikafuatiwa na semina ya Katiba Inayopendekezwa”.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa, “Wakati akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu katiba hiyo mpya, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi ambaye pia ni Mjumbe wa NEC kupitia Wazazi (anatajwa), aliwadokeza wajumbe kuhusu miswada hiyo miwili na kuwa ni mhimu”.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwenda kwa mmoja wa kigogo mwandamizi wa CCM, miswada hiyo ni baada ya serikali kubaini kwamba magazeti mengi nchini, hivi sasa yanatumiwa vibaya na wapinzani kufanya uchochezi kwa kuandika uzushi na uongo kwa makusudi dhidi ya CCM na serikali yake.

Naibu waziri huyo, aliyataja magazeti hayo “yanayokera” CCM na Serikali yake kuwa ni Mwananchi, Mtanzania, Nipashe na Tanzania Daima, na kufafanua kuwa serikali imeamua kuwasilisha miswada hiyo bungeni katika mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri unaoendelea.

“Alisema gazeti lolote litakaloandika uongo, uzushi ama uchochezi, litachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufungiwa “mara moja” na kusema uhuru wa magazeti hapa nchini umevuka mipaka,”inasomeka taarifa hiyo.

Inaongeza kuwa, naibu waziri huyo, alitolea mfano wa Kenya aliyosema ina magazeti matatu tu na kwamba Tanzania ina utitiri wa vyombo hivyo vya habari na sasa vinatumiwa vibaya, kinyume cha malengo yaliyokusudiwa.

error: Content is protected !!