
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tabora kimeiomba serikali kuwapa kipaumbele wazawa katika miradi ya ujenzi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora…(endelea).
Kauli hiyo imetolewa na Hassan Wakasuvi, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Tabora wakati akiongoza kamati ya siasa ya mkoa huo kukagua ujenzi wa Barabara ya Urambo – Kaliua.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 28, inajengwa na kampuni ya wazawa ya Samota.
Wakasuvi amesema, serikali ikiendeleza utaratibu wa kuwapa kazi wazawa, kwa kiwango kikubwa itapunguza gharama za ujenzi.

“Kampuni za wazawa zikipewa kazi, serikali itapunguza gharama kwa sababu, haitakuwa gharama kusafirisha vifaa vya ujenzi,” amesema.
Amesema, wakandarasi wazawa wameonesha uwezo na uaminifu katika ujenzi hasa wa barabara, na kwamba kwa kuwatumia wazawa kunainua uchumi wa nchi.
“Tunaomba kutolewa kipaumbele kwa wazawa kwa kuwa, kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mitaji yao,” amesema Wakasuvi.
Salum Abdallah, mkurugenzi wa kampuni hiyo ameishukuru serikali kwa kuwaamini kwa kuwapa mradi huo wenye thamani ya Sh. 38.7. bilioni.
Hiyo ni sera ya CCM? Ni kauli ya CCM au ya mwenyekiti wa mkoa anayetaka apewe zabuni ya ujenzi?
Uzawa ina maana gani? Ni sera ya CCM au ni ukaburu kama alivyosema Mwalimu?
Waandishi msitupotoshe