January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM wazidi kuweweseka, wananchi wawaonya

Spread the love

BAADHI ya wananchi jimbo la Dodoma Mjini wamewataka viongozi wa kampeni pamoja na mgombea ubunge wa CCM, Antony Mavunde kuweka sera zao hadharani badala ya kujadili matatizo ya mtu binafsi. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kwa nyakati tofauti wamesema kwamba kwa sasa CCM wameishiwa sera na matokeo yake wanaweweseka na kuanza kuingilia uhuru wa mbu binafsi jambo ambalo wamesema halina maana kwa jamii.

Wananchi wamelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na mwanasheria wa CCM, Antony Kanyama na mgombea Ubunge kupitia CCM, Antony Mavunde kudai kuwa Mgombea Ubunge kupitia Chadema jimbo hilo, Benson Kigaila hana mke wala nyumba.

Mkazi wa jimbo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Juma Khamisi ameliambia MwanahalisiOnline, watanzania wanahitaji mabadiliko na siyo mtu kaoa au la.

“Tunawashangaa watu wa CCM kuweka sera pembeni na kuingilia matatizo ya mtu binafsi kwa sasa viongozi wa CCM wanashindwa kueleza watawafanyia nini kwa wananchi wa Dodoma na badala wanajikita katika mambo binafsi.

“Kama Kigaila (Benson) ana mke au hana mke sisi wananchi inatusaidia nini tunachotaka ni maendeleo, hawa jamaa ni kama wanaweweseka tu,”amesema Khamisi.

Naye dada ambaye ni muuza mboga sokoni hakutaka jina lake liandikwe, amesema kama kuoa au kuolewa ni kipimo cha utendaji taifa lisingekuwa masikini kwani Rais wa nchi na Waziri mkuu wana wake na wameoa.

Hata hivyo alienda mbali zaidi kwa kusema wapo viongozi wakubwa wa nchi hapa Tanzania wana watoto wengi wa nje kwa maana hiyo hata hao wamepora wake za watu.

Kwa Upande wake Mgombea ubunge jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chadema, Benson Kigaila amabaye anatuhumiwa alisema hizo ni siasa za maji taka.

Amesema wananchi wanataka kujua matatizo yao yatatatuliwaje, siyo Mbunge kuwa na mke au la.

Hata hivyo amesema Mavunde ni mwanasheria na Kanyama ni mwanasheria je wamepelekewa hiyo kesi au huyo mke ni wa kwao?

Hata hivyo amesema wapo vijana wengi ambao hawajaoa na kama kuoa ni kipimo cha utendani wapeleke wake zao wawapatie vijana wawaoe kwa zamu ili wapate nguvu na ujasiri wa utendaji.

“Unajua mimi sitaki kujibu hoja ya kitoto kama uongozi ni kuwa na nyumba mbona Kikwete ana nyumba lakini umasikini umeisha, mbona aliyekuwa Mbunge Ephrahim Madeje alikuwa na nyumba kama siasa ni hizo mbona inasemekana Mgombea ubunge CCM jimbo la Dodoma kauza nyumba ya baba yake, Je anategemea kuikomboaje kama siyo kuwaibia wananchi.

“Mavunde ni wakili ambaye amesaidia sana wananchi wa Dodoma kuporwa ardhi yao na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) sasa mtu wa jinsi hiyo hawezi kuwaongoza wana Dodoma kwa uaminifu,” amesema Kigaila.

error: Content is protected !!