May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM, wastaafu watakiwa kutubu

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  kimewataka viongozi wastaafu na walioko madarakani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na wa serikali, kuwaomba radhi Watanzania. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam… (endelea).

Ni kutokana na dosari zilizojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 ili kuleta utengamano wa Taifa.

Wito huo umetolewa leo tarehe 11 Aprili 2021, mkoani Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, wakati akilihutubia Taifa.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, viongozi hao wanapswa kuomba radhi kwa kosa la kufumbia macho dosari hizo.

“CCM huwa kinawaza nini na kuzungumza nini katika vikao vyake?  Nimetafakari sana je viongozi wake wastaafu waliweza vipi kushiriki huku watu wakilalamika. Kuna sehemu hawa nao wamelibaka sana Taifa letu hawastahili kubeba dhamana ya maisha.

“Angalau Taifa lingeombwa  msahama na viongozi wastaafu wa CCM, ambao waliweza kufurahi na  kushangilia ubunge na udiwani ambao haukuwa haki yao, huku wakijua katika hatua za awali hawakushinda uchaguzi. Hata kama ni kuleta utengamano wa Taifa, tunahitaji apology (kuomba radhi) kwa nchi na Watanzaia,” amesema Mbowe.

error: Content is protected !!