Spread the love

 

DANIEL Chongolo, Katibu Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemjulia hali aliyekuwa mbunge wa Mikumo mkoani Morogoro kupitia CHadema, Joseph Leonard Haule maarufu Profesa Jay, aliyelazwa Hospital ya Taifa Muhimbili (MNH). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Chongolo akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka wamekwenda kumjulia hali msaani huyo leo Alhamisi, tarehe 10 Februari 2022.

“Tumemuona ndugu yetu (Prof Jay), hali yake inazidi kuimarika, tumshukuru Mungu lakini niwashkuru madaktari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kumhudumia,” amesema Chongolo na kuongeza:

“Pamoja na mchango huu wa kuwezesha matatibu lakini kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan niwahakikishie tutaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha matibabu yanaendelea vyema huku tukiendelea kumuombea apone haraka.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *