August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM wakomba hoteli 306 Dodoma

Spread the love

JUMLA ya hoteli 306 sawa na vyumba 3331 zimemekodiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya mkutano mkuu wa chama hicho ambao unalengo la kumkabidhi Rais John Magufuli kushika nafasi ya unyekiti, anaandika Dany Tibason.

Hayo yalielezwa na msemaji wa CCM, Christopher  ole Sendeka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa chama hicho unaokusudiwa kufanyika 23 Julai mwaka huu.

Amesema, katika kuhakikisha maandalizi yanafanyika na wajumbe wote wanafika katika mkutano huo, kwa sasa pesa za kuwasafirisha wajumbe kutoka mikoani tayari zimeandaliwa ikiwa ni pamoja na kukodi mabasi ya kutosha.

Sendeka amesema, kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Mwenyekiti wa CCM ambaye kwa sasa ni Dk. Jakaya Kikwete alitakiwa kuendelea hadi mwaka kesho.

“Lakini kutokana na desturi ambayo imezoeleka na ipo ndani ya chama, mwenyekiti wa sasa ambaye ni Jakaya Kikwete atalazimika kujiuzulu ili Rais John Magufuli aweze kupigiwa kura za ndiyo au hapana.

“Nafasi ya uenyekiti haiombwi bali kamati kuu inapendekeza jina ambalo hupelekwa katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na jina hilo hupigiwa kura na Halmashauri Kuu ambapo anatakiwa kupata nusu ya kura zote.

“… na ikitokea hakupata nusu ya kura za wajumbe wote, mtu huyo anakuwa hajashinda kuwa mwenyekiti wa chama taifa,” amesema Ole Sendeka.

Amesema, mara baada ya kumpata mwenyekiti wa CCM taifa, katibu mkuu na msaidizi wake pamoja na viongozi wengine watajiuzulu kwa lengo la kumwacha mwenyekiti kupanga timu yake ya sekretarieti mpya ya chama ambayo ataweza kufanya nayo kazi kwa lengo la kuimarisha chama.

“Tarehe 25 Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana kwa niaba ya sekretarieti nzima ya chama ili yeye na sekretarieti nzima tuweze kujiuzulu kumpisha John Magufuli, mwenyekiti ili aweze kuunda safu mpya atakayopenda kufanya nayo kazi ili kuleta nguvu nyingine mpya kadri itakavyompendeza ” amesema.

Amesema, viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM watawasili mjini Dodoma Julai 21 mwaka huu kwa kuanza kikao na wajumbe wengine wa mkutano mkuu wa taifa watawasili Julai 22 mwaka huu.

Amesema, kabla ya mkutano mkuu wa taifa watakuwa na vikao ambavyo alivitaja kuwa Julai 19 kutakuwa na sekretarieti ya halmashauri kuu,21 Julai Kamati kuu ya halmashauri kuu,22 Julai Halmashauri kuu ya taifa na 23 Julai utakuwa mkutano mkuu maalum wa taifa.

Kuhusu ilinzi Ole Sendeka amesema, ulinzi umeimalishwa na kila jambo lipo sawa kwa ajili ya kufanya mkutano.

Kuhusu kauli ya UVCCM kujinadi kuwa, watalinda mkutano wa CCM amesema hawana uwezo wa kulinda mkutano huo kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yao vizuri.

“UVCCM hawana uwezo wa kulinda mkutano na walinde ili iweje, na kwa sasa sitaki kuongelea jambo hilo kwani CCM tumeishavuka lengo la kujibiza,” amesema Sendeka.

 

error: Content is protected !!