March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CCM wajipanga kumrudisha Rais Magufuli 2020

Mgombea Urais wa CCM, John Magufuli (kushoto) akiwa na mgombea mwenza wake Samia Suluhu

Spread the love

MWENYEKITI wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa, Dk. Edmund Mndolwa amewaagiza wajumbe wa Baraza Kuu la Wazazi kujipanga kikamilifu ili wamrudishe madarakani Rais Dk. John Magufuli 2020. Anaripoti Danson Kaijage, kutoka Dodoma … (endelea).

Dk. Mndolwa aliyasema hayo jijini hapa wakati akifunga mkutano wa baraza kuu la wazazi Taifa akisema mwaka 2019 ni mwaka wa ukombozi wa kuhakikisha wanashinda chaguzi zote zijazo.

“Wenzetu wamechoka wako hoi bin taabani na sera zao ni matusi wakilenga kutuzoofisha lakini hawatatuweza lazima tuhakikishe tunawachapa, hata wakijificha uvunguni tuwafuate.

“Huu ni mwaka wa ukombozi kwa CCM kuhakikisha tunashinda uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, uchaguzi mkubwa 2020 katika nafasi ya udiwani, ubunge ili kuhakikisha Dk. John Magufuli anarudi madarakani,” alisema Dk Mndolwa.

Baraza hilo pia lilifanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi zilizo wazi ambazo ni mjumbe wa halmashauri kuu taifa na mjumbe wa baraza kuu Taifa.

Katibu wa Jumuiya hiyo, Erasto Sima alisema Waliochaguliwa ni Galali Wabanhu mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa akichukua nafasi ya Kitwana Komanya ambaye aliteuliwa kuwa DC wa Tabora na Rajab Mwilima mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa akiziba nafasi ya aliyekuwa mbunge wa Korogwe, Steven Ngonyani ambaye alifariki dunia.

error: Content is protected !!