July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CCM waifanyia mbaya CUF

Spread the love

YOWE linapigwa na Chama cha Wananchi (CUF) dhidi ya rafu zinazochezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Faki Sosi.

Ahmed Mbonde, Diwani wa Kata ya Kilindoni (CUF) wilayani Mafia katika Mkoa wa Pwani analalamika kwamba, CCM kinakwaza maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Mafia.

“Itikadi za vyama vya siasa zinasababisha maendeleo ya jimbo hili kudumaa. Hapa madiwani wa CCM wanawatenga wale wa CUF kutokana na hasira za kisiasa,” anasema Mbonde.

Akizungumza na Mwanahalisi Online anasema kuwa, ubinafsi ndio utakaorudisha nyuma maendeleo.

Katika kadhia hiyo Mbonde anadai kuwa, Mbaraka Dau, amekuwa akiendesha mapambano na CUF.

“Bwana huyu amekuwa akidai sisi CUF ni watu wadogo kwake na hivi ni wapinzani ndio hataki kutusikia,” amedai.

Kwa habari zaidi soma gazeti la MwanaHALISI la kesho.

error: Content is protected !!