KAMATI ya Siasa ya CCM mkoa wa Dodoma imeiagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD), kuhakikisha inapeleka vifaa tiba na dawa katika vituo vya afya vilivyokamilika. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Pia amewataka wauguzi na wataalam wa afya kutoa huduma kwa kuzingatia weledi kama ambavyo kanuni za taaluma yao zinavyoelekeza.
Agizo hilo lilitolewa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati wa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika miradi inayotekelezwa na serikali.
Mkanwa alisema, inashangaza kuona fedha za ujenzi wa vituo zinatolewa siku moja na fedha za vifaa tiba na dawa, lakini MSD wanashindwa kupeleka dawa kwenye vituo baada ya kukamilika.
Alisema, huo ni uzembe mkubwa na hauendi sambamba na dhamira ya Rais, Dk.Magufuli ya kuwaletea wananchi maendeleo hasa katika kuboresha sekta ya afya nchini.
“Nawaagiza MSD mpeleke vifaa mara moja katika vituo vya afya vilivyokamilika, ili viweza kufanya kazi na wananchi wapate huduma kama ilivyokusudiwa,” alisisitiza Mkanwa.
Kuhusu watumishi wa afya, alisema wakifanya Kazi yao kwa upendo, huruma na uadilifu wananchi watatamani kufika katika kituo hicho kuhudumiwa, lakini wakiwa wanawatolea lugha chafu na za matusi watavunjika moyo hivyo itakuwa sawa na bure kwa kujenga nyumba nzuri na wakaaji.
“Ninyi mko Ikulu hivyo kituo chenu kinatakiwa kuonyesha mfano kwa kuwa kituo bora kabisa, na si kujaa malalamiko na sifa mbaya kutoka kwa wagonjwa,” alisema.
Aliwapongeza kwa ujenzi wa majengo na zuri na yenye ubora ambavyo yanadhihirisha thamani ya fedha iliyotolewa na serikali huku akiwataka kuyatunza vizuri.
Mkanwa akiwa Wilayani Kongwa pia alipata fulsa ya kukagua kituo cha afya Ugogoni kilichopo Wilayani Kongwa ambacho kimejengwa kwa thamani ya Sh.milioni 4 ambazo zimetolewa na serikali.
Baada ya kumaliza kukagua kituo hicho pamoja na kuwapongeza kwa ujenzi wa viwango vya ubora wa hali ya juu tofauti na wilaya Nyingine alizopita alimtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha ujenzi ifikapo Februari 28 na kukabidhi Kazi hiyo kwa uongozi wa wilaya.
Pia alikagua majengo ya mradi wa machinjio ya kisasa ya kuku katika eneo Mbande njia panda ya Kongwa na mradi wa maji katika mji wa Kongwa na kutoka maelekezo mbalimbali za uboreshaji wa miradi hiyo.
Sambamba na hilo, alielekeza kutolewa vyeti na motisha kwa wajumbe wa kamati wanaosimamia ujenzi wa majengo ya miradi ya serikali ili kuwapa molali ya kufanya Kazi hiyo kwa umakini.
Awali akikaribisha ujumbe wa kamati hiyo ya Siasa, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi, aliushukuru serikali kwa kuwapatia fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo vituo vya afya.
Ndejembi, alisema anaiona dhamira njema ya Rais, Dk.Magufuli ya kuwaletea wananchi maendeleo na kwamba katika wilaya ya Kongwa walipokea kiasi cha Sh.milioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa vituo viwili vya afya ambavyo ni Mlali na Ugogoni.
Leave a comment