October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM wafurika kuchukua fomu za Ubunge Moshi Mjini

Mkurugenzi wa Ibraline Foundation , Ibrahim Shayo akiingia kwenye gari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Moshi mjini katika ofisi za Chama cha Mapinduzi(CCM)

Spread the love

MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Moshi Mjini wamefurika kwenye ofisi ya chama hicho wilaya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge. Anaandika Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Leo tarehe 14 Julai 2020, ni siku ya kwanza kwa watia nia wa CCM kuchukua fomu za kuomba kupitishwa na chama hicho, zoezi hilo linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 17 Julai 2020.

Mpaka kufika saa 8 mchana wa leo, jumla ya makada saba walikuwa tayari wamechukua fomu huku taarifa zikieleza, wengine wapo njiani kujitokeza.

Waliochukua fomu mpaka sasa ni Mkurugenzi wa Ibraline Foundation na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Mkoa wa Kilimanjaro, Ibrahim Shayo.

Wengine ni Priscus Tarimo, Issah Wilium, Noel Nko, Mwalimu Evans Mghase, Faraji Swai na Alfa Kiwango. Kwa leo, zoezi hilo linatarajiwa kuhitimishwa saa 12:00 jioni.

error: Content is protected !!