June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM wachukua majimbo yote Dodoma

Spread the love

WAKURUGENZI wa halmashauri mbalimbali katika majimbo ndani ya mkoa wa Dodoma wametangaza matokeo ya majimbo yote ambayo yameenda kwa Chama cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Majimbo hayo ni pamoja na Dodoma Mjini, Chemba, Mpwapwa, Kondoa, Kondoa Vijini, Bahi, Kongwa, Chilonwa na Mtera.

CHEMBA

Katika jimbo la Chemba Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (CCM) ameshinda jimbo hilo kwa kupata kura 50,223, huku Ngimba Akley(CUF) akipata kura 18,908.

Wengine ni Kataa Ibrahim(ACT) ambaye alipata kura 1,873.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Dk. William Mafwele kura zilizopigwa ni 76,466.

Katika Jimbo hilo kuna jumla ya kata 26, ambapo kata 23 zimechukuliwa na CCM, huku kata 2 zikienda kwa Chadema na CUF ikiambulia kata moja.

KONGWA

Kwa upande wa Jimbo la Kongwa, aliyekuwa Naibu Spika, Job Ndugai (CCM), ameibuka kidedea kwa kupata kura 73,165 sawa na asilimia 76.89 akimshinda mpinzani wake Ngobei Fremont aliyepata kura 20335 sawa na asilimia 21.37.

Wengine ni Noel Mgasa (ACT) 1510 sawa na asilimia 1.59 na Eliud Masulu aliyepata kura 147 sawa na asilimia 0.15.

Katika Jimbo hilo, kata zote 22 zimechukuliwa na CCM.

MPWAPWA

Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje (CCM) ameshinda kwa kupata kura 32,208 sawa na asilimia 74.46 akimshinda mpinzani wake Ezekiel Chisinjila (Chadema), aliyepata kura 11,048 sawa na asilimia 25.04.

Matokeo hayo ni kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Mohamed Maje.

Kwa mujibu wa msimamizi huyo, Kata zote 15 zimechukuliwa na CCM.

KONDOA VIJIJINI

Katika jimbo la Kondoa Vijijini, Dk. Ashatu Kijaji (CCM), ametangazwa mshindi wa ubunge katika jimbo hilo kwa kupata kura 37,795.

Yasini Shabani (CUF), akipata kura 23,570, Saidi Njuki (ACT), akipata kura 2,469 na Issa Swalehe (UDP) akipata kura 10.

Msimamizi wa Uchaguzi, Hussein Issa, amesema, kwa upande wa matokeo ya udiwani CCM imepata viti 15, CUF 4 na chadema 2.

MTERA

Jimbo la Mtera, Livistone Lisinde (CCM), ametetea nafasi yake tena baada ya kuibuka kidedea na kuwabwaga wapinzani wake.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Saada Mwaruka, amesema jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 55,768, kura halali ni 54,223, kura zilizoharibika zilikuwa 1545.

Katika kura hizo Lusinde aliibuka na kura 47,147 huku Christopher Nyamwanji (Chadema), akiambulia kura 6275.

Kwa upande wa Udiwani amesema kati ya kata 22 zilizopo katika jimbo hilo, CCM imechukua kata 21 huku Chadema wakiondoka na kata 1.

CHILONWA

Kwa upande wa jimbo la Chilonwa, Joel Mwaka (CCM), aliibuka na ushindi baada ya kupata kura 39,557, nafasi ya pili ikichukuliwa na John Chigongo (Chadema), aliyepata kura 4,206.

Katika jimbo hilo jumla ya kata 14 zilizopo zote CCM iliibuka na ushindi wa viti vya udiwani.

KONDOA

Katika jimbo la Kondoa, Edwin Sanda (CCM), ameibuka mshindi baada ya kupata kura 13333 akifuatiwa na Ally Kambi (CUF) aliyepata kura 6783.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi, Samwel Simbira, amesema kati ya kata nane za jimbo hilo CCM wameshinda kata 7 huku moja ikienda upinzani.

BAHI

Kwa upande wa jimbo la Bahi, Omary Badwel ameshinda na kutetea kiti chake baada ya kupata kura 48,792 kati ya kura 61,965 zilizopigwa.

Badwel aliibuka kidedea na kuwabwaga wapinzani wake ambao ni Mathias Lyamunda (Chadema), aliyepata kura 12,527 huku Habel Kaka (ACT) akiambulia kura 646.

KIBAKWE

Jimbo la Kibakwe, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madin, George Simbachaweni (CCM), alitwaa ushindi wa kishindo akipata kura 37,327 sawa na asilimia 81.55 kati ya kura 45,774 zilizopigwa.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa mgombea wa Chadema, Mzinga William, aliyepata kura 8,447, sawa na asilimia 18.45 mbunge wa kwa upande wa viti vya udiwani udiwani katika jimbo hilo, CCM wamechukua kata zote 18.

DODOMA MJINI

Jimbo la Dodoma mjini lilitwaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde baada ya kupata kura 84,512 na dhidi ya Benson Kigaila (Chadema), aliyepata kura 42,140.

error: Content is protected !!