May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM wabanana mbavu

Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Iringa kimetengeneza utaratibu mpya wa kuwapima madiwani na wabunge wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Sasa mbunge na diwani kwenye mkoa huo, atatakiwa kukutana na wananchi kila baada ya miezi mitatu na kueleza nini amefanya kwenye kipindi hicho.

Uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao maalumu cha chama hicho kilichowakutanisha wabunge na madiwani hao ambapo Dk. Abel Nyamahanga, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa amesema “itasaidia kufuatilia ahadi zao.”

Dk. Nyamahanga amesema, chama hichi kimeweka utaratibu huo kuwalazimisha viongozi hao kutoa taarifa lakini pia kuonesha mafanikio ya uchapaji kazi wao.

Amesema, hatua hiyo pia itaongeza imani ya wananchi kwa CCM na kurahisisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa chama hicho.

Kikao hichi pia kimehudhuriwa na Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Pinda amewataka wabunge na madiwani hao kuwa karbu na wananchi ili kujua changamoto zinaqzowakabilia na kujua namna ya kuzitatua.

error: Content is protected !!