August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM waanza kumgeuka Magufuli

Spread the love

HALI mbaya ya uchumi inaanza kuwaweka pamoja wabunge wa Tanzania, tayari wameanza kumshughulikia Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Ilikuwa minong’ono kwa mbunge mmoja mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulalamikia namna uchumi wa nchi unavyoyumba miezi michache tangu Rais Magufuli kuingia madarakani, sasa wanaanza kujitokeza na kuungana na wabunge wa upinzani.

Goodluck Milingwa, Mbunge wa Ulanga Mashariki amevunja ukimwa ndani ya ukunbi wabunge jana na kuanza kunyooshea kidole utawala wa Rais Magufuli kwamba, wananchi wanatopea kwenye umasikini.

“Hali ya maisha ni ngumu sana, namuomba Muheshimiwa Rais hapo aliposhika kwa sababu si mahali pake, hali imekuwa ngumu sana,” amesema Milingwa akilalamikia umasikini unaokuwa kwa kasi chini ya utawala wa Rais Magufuli.

Alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Taarifa ya Mwaka 2016. Muswada huo uliwasilishwa juzi na Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria.

Kauli hizo zilikuwa zikitolewa na wabunge ama wadau wa vyama vya upinzani, taasisi na wasomi mbalimbali nchini.

Milingwa anaungana na mailioni ya Watanzania wanaolalamikia maisha kuwa magumu zaidi kuliko wakati wa Utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. Jakaya Kikwete.

Ugumu wa maisha sasa unatambuliwa rasmi na Rais Magufuli ambapo hivi karibuni alidai kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuchangia hali hiyo kutokana na kutoa fedha zao benki na kukaa nazo majumbani wao.

Mtikisiko wa uchumi nchini upo dhahiri ambapo juzi Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo alinukuu taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ikionesha namna wananchi wanavyotopea kwenye umasikini katika uongozi wa Rais Magufuli.

Kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya kiuchumi miezi michache Rais Magufuli kuingia madarakani, baadhi ya hoteli nchini zimefungwa.

Pia wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam wamehamisha mizigo yao na kutumia bandari zingine, madereva wa malori wakiachwa bila kazi huku kiasi kikubwa cha fedha zinazotokana na kodi zikipotea.

Katika taarifa ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliyoinukuu kutoka BoT na baadaye kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ameeleza;

  1. a) Taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake (Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba – Desemba 2015 ) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari – Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%. Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%.
  2. b) Shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita. Hii ina maanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama Mapinduzi iingie madarakani
  3. c) Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 ilikuwa 13.8% lakini ukuaji wa sekta hii katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.
  4. d) Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie wanaowauzia chakula.
error: Content is protected !!