Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CCM Vyuo Vikuu walia na rushwa ya ngono
Habari za Siasa

CCM Vyuo Vikuu walia na rushwa ya ngono

Zainabu Abdallah, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo Vikuu la Chama Cha Mapinduzi
Spread the love

NEEMA Mfugale, Katibu wa Shirikisho la Vyuo Vikuu la Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma amesema, rushwa ya ngono ni changamoto kubwa inayokwamisha wanafunzi wa kike vyuoni kukubali kuwania nafasi mbalimbali ndani ya CCM, anaandika Dany Tibason.

Mfugale ameyasema hayo jana mbele ya Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT) uliolenga kusikiliza kero za wanafunzi wa kike ambao ni wanachama wa CCM katika vyuo vikuu.

“Wanafunzi wa kike wanashindwa kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja rushwa ya ngono na vitisho kila wanapotaka kugombea nafasi hizo,” alisema Neema.

Ameongeza kuwa, “….Lakini pia wanafunzi hawa wa kike wanakabiliwa na changamoto ya kutokujitambua, uoga na tabia ya kutopendana jambo ambalo linawakatisha tamaa ya kugombea nafasi mbalimbali.”

Neema amedai kuwa bado wanafunzi wa kike hawana ujasiri wa kukabiliana na fitna pamoja na hujuma katika michakato ya uchaguzi, ndiyo maana wamekuwa wakisuasua kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali.

Akijibu hoja hizo, Dk. Tulia alisema suala la rushwa ya ngono lipo na linafahamika lakini inategemea na utashi binafsi wa msichana pamoja na msimamo alionao.

Dk. Tulia amesema, “Ili wanafunzi wa kike na wanawake kwa ujumla waweze kuepukana na tatizo la rushwa ya ngono katika chaguzi za ndani ya CCM ni lazima wawe na misimamo pamoja na kujiamini katika kile wanachokifanya.

“Jinsi mdada alivyojiweka ndiyo inaweza kumfanya kuwa mhanga wa rushwa ya ngono. Kwa mfano kama mtu hatakuwa na bidii ya kusoma kamwe hawezi kujiamini wala kuwa na uhakika na uwezo wake na hivyo ni rahisi kujiingiza katika rushwa ya ngono.”

Dk. Tulia amewaasa wanafunzi wa kike akisema, “Ukikubali kutoa rushwa ya ngono kwa kiongozi wa chama ili upate nafasi ya uongozi utafanya hivyo kwa watu wangapi na utakuwa binti wa aina gani? Ni vyema kujiamini na kuwa makini.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!