October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM Ubungo wamdhamini Magufuli, wasema anatosha

Spread the love
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamesema, mgombea wa chama hicho wa nafasi ya Urais, Dk. John Pombe Magufuli anatosha na wala hana mpinzani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe  18 Juni 2020 na Mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja wakati akiwaongoza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani humu kujaza fomu za kumdhamini Rais Magufuli.
Jana Jumatano, Rais Magufuli alianza safari ya kusaka kuwaongoza Watanzania katika muhula wa pili wa miaka mitano ijayo kwa kuchukua fomu za Urais ndani ya CCM.
Fomu hizo alizichukua ofisi za makao makuu ya CCM, jijini Dodoma na kukabidhiwa na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa chama hicho.
Baada ya kukabidhiwa, alisema atazunguka nchi nzima kutafuta wachamini 250 kwa mujibu wa masharti huku akidokeza, atafanya haraka ili kuzirejesha mapema.
Taarifa ilitolewa leo Alhamisi tarehe 18 Juni 2020 na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi, imesema, wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya Wilaya wameshiriki shughuli hiyo  kwa ngazi ya wilaya.
Mbali na mwenyekiti wa wilaya, wengine waliokuwepo ni; Katibu wa CCM Wilaya Chifu Sylevester Yared pamoja na kamisaa wa chama ambaye pia mi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori.
Akizungumza na wajumbe hao, Mgonja amesema, hatua hiyo ni heshima kubwa kwao kwani wanaamini Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maoni na ataendelea kuifanyia mema Tanzania.
“Ubungo tunasema kwa kauli moja kwamba Magufuki anatosha, tunamwamini na tumemkubali na tunahakika atatuvusha tena kama alivyotuvusha,” amesema Mgonja
Amesema, “miakamitano ya kwanza hakika ametenda kazi kubwa na kila Mtanzani ni shuhuda nasi Ubungo alitupendelea kwa kuwa na miradi mikubwa ikiwamo Ubungo Inter Change pamoja na barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha kwetu ni heshima kubwa.”
Mwenyekiti huyo amesema,”si hili tu hata ukiangalia miradi ya maji, ujenzi wa shule na zahanati pamoja na hospitali za wilaya nasi Ubungo ni sehemu ya wanufaika wakubwa wa miradi hii.”
“Kwa hakika Rais Magufuli ameitendea haki CCM na aliahidi na ametekeleza kila sekta kama ilani ya chama ilivyoelekeza,” amesema Mgonja
Kwa upande wake, DC Makori amesema,”kazi kubwa iliyofanywa na Rais Magufuli katika Wilaya ya Ubungo ni kilelezo tosha kwamba anastahili kuungwa mkono na kila Mtanzania mpenda maendeleo.
Jumla wa wajumbe 75 wamemdhamini ngazi ya wilaya huku fomu hizo zikishushwa ngazi ya kata ambapo kwa Ubungo atadhaminiwa na wanachama zaidi ya 15,000.
error: Content is protected !!