January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM, Upinzani watakiwa kujiandaa kisaikolojia

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania Sheikh Mohamed Issa (mwenye kanzu nyeupe)

Spread the love

UMOJA wa Wanazuoni wa kiislam Tanzania watoa tamko la kuomba vyama vya siasa kukujiandaa kwa kupokea matokea ya uchaguzi mkuu. Anaandika Hamisi Mguta, DSJ …  (endelea).

Tamko hilo lilitolewa na taasisi hiyo kwa madiwani,wabunge, wawakilishi na Rais pamoja na wananchi kwa ujumla ili kuleta amani kufuatia kipindi cha uchaguzi. 

Akisoma tamko hilo kwa niaba ya umoja huo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania Sheikh Mohamed Issa amesema wamelazimika kutoa tamko hilo kutokana na hali inayojitokeza ambapo malalamiko ya wagombea kutotendewa haki, matumizi ya rushwa kama kishawishi cha kuchaguliwa pamoja na kauli za wanasiasa zinazoashiria hatari kuanza kusikika waziwazi.

Sheikh Issa Amesema kuvamiwa kwa vituo na polisi kuuwawa na siraha kuibiwa na watu wasiojulikana, matumizi ya rushwa na vurugu katika kampeni za uchaguzi kuanza kujitokeza pamoja na matukio yanayozidi kila uchao ya wananchi kukosa ustahamilivu na kujichukulia hatua mikononi ni miongoni mambo wanayoyaona kuleta hatari.

…amewaambia wanahabari kuwa zipo kauli ambazo zinaashiria kujiandaa kwa wizi wa kura, jambo ambalo ni hatari kwa amani na utulivu wa nchi yetu huku akinukuu kauli iliyotolewa na kiongozi mmoja wa siasa ambayo ilinukuliwa pia na vyombo vya habari “CCM itashinda tu hata kwa goli la mkono” na kumpongeza Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva kwa kuikataa kauli hiyo na kuahidi kuwa tume haitaruhusu jambo kama hilo kutokea.

amesema kauli nyingine inayoashiria hatari ni kauli iliyotolewa na mmoja wa kiongozi wa chama pinzani (UKAWA)alipokua akihutubia jijini mwanza aliliambia jeshi la polisi nchini kwamba “Hatutapiga magoti na kuomba, kama ushindi utapatikana kwa njia ya halali hatuna tatizo, lakini tukiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo tutasema polisi mtatusamehe, mabomu hayatatosha” hivyo ametaka vyombo vya habari , viongozi wa dini pamoja na wananchi kutanguliza mbele maslahi ya Taifa kuliko kitu chochote na kutumia njia za amani kutatua migogoro itakayojitokeza.

Aidha, ameiomba tume ya uchaguzi (NEC) kusimamia uchaguzi kwa makini ili uwe huru na haki.

error: Content is protected !!