Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM Mwanza wamgomea Rais Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

CCM Mwanza wamgomea Rais Magufuli

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire. Picha ndogo baraza la madiwani wa jiji hilo.
Spread the love

PAMOJA na Rais John Magufuli kuwataka Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire, Mkuu wa Mkoa, John Mongela na Mkurugenzi wa jiji hilo, Kiomoni Kibamba kwa kuwa wote ni wanachama wa CCM, hali imezidi kuwa mbaya baada ya madiwani wa baraza hilo kushikilia msimamo wao wa kutokuwa na imani na meya huyo, anaandika Moses Mseti.

Madiwani 18 kati ya 24 wa baraza la madiwani wa Jiji hilo, tayari walishasaini waraka wa kutokuwa na imani na Meya huyo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Madiwani hao wanamtuhumu Bwire, kwamba baada ya kuingia madarakani, alianza kupora viwanja vya halmashauri hiyo ikiwemo viwanja vilivyo kata ya Mahina anapoendelea kujenga hospitali yake iliyopo karibu na shule yake za Alliance.

Tuhuma nyingine, ni kwamba amekuwa akifunga ofisi muda wowote anaoutaka na kwenda kufanya shughuli zake binafsi, kutumia gari la Jiji kwenda kufanya shughuli zake na kushinikiza kuwekewa mafuta na kuisababishia halmashauri hasara.

Tuhuma nyingine zinazomkabiliwa Bwire ni zile za kumtuhumu Mkurugenzi wa Jiji  hilo, Kibamba kwamba alifanya njama za kutaka kumwekea kitu kinahodhaniwa sumu ofisini kwake kitendo ambacho kimezorotesha utendaji kazi katika halmashauri hiyo.

Hoja hiyo ya kutokuwa na imani na Meya imeibuliwa leo dakika nne mara baada ya wimbo wa kuombea baraza la madiwani na ulipofika muda wa kuanza kwa bara hilo na Diwani wa Kata ya Mkolani Donatha Gapi, aliyenyoosha mkono na kuomba mwongozo.

Pia Meya huyo anatuhumiwa kuomba fedha kutoka kwa Kibamba, pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa Jiji hilo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Adam Mgoyi, aliyemuomba zaidi ya Sh. 20 milioni.

Licha ya Oktoba 30 mwaka huu, Rais John Magufuli kuagiza pande hizo mbili kukaa chini na kumaliza mgogoro huo, leo Novemba 2 kikao cha baraza la madiwani kiliketi lakini kilishindwa kuendelea kutokana na madiwani kushikilia msimamo wao wa kutokuwa na imani na Meya huyo.

Madiwani wa CCM baada ya kupata taarifa meya ataongoza kikao hicho kilichotarajiwa kufanyika leo saa nne asubuhi walikazimika kutoka nje ya ukumbi na kuanza kukaa makundi makundi ambapo baada ya saa moja waliingia katika ofisi ya mkurugenzi.

Baada ya kuiingia katika ofisi ya mkurugenzi na kuanza kufanya kikao cha ndani kilichoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, kuzungumzia mgogoro huo, ambapo inadaiwa baadhi ya madiwani waliendelea kushikilia msimamo wao wa kutoendelea kufanya kazi na Meya huyo.

Kikao hicho kilichodumu kwa saa mbili, taarifa zinasema kiliazimia Meya kung’atuka katika nafasi hiyo kwa manufaa ya wananchi wa jiji hilo, huku madiwani wanne wa Chadema wakiendelea kukaa kwenye ukumbi wa mikutano na wao baadae iliwazimu kuzungumza na wanahabari.

Wakizungumza kufuatia tukio hilo Madiwani wa Chadema, Jonh Pambalu na Samweli Range, kwa pamoja walisema mgogoro huo unasababisha maendeleo ya jiji la Mwanza na Taifa kwa ujumla kushuka kutokana na vikao vya baraza la madiwani kushindwa kufanyika.

Walisema mgogoro huo, unazidi kuathiri shughuli za kimaendeleo ya jiji hilo huku akidai kwamba umefika wakati wa mamlaka husika kuangalia namna ya kuutatua mgogoro huo.

“Leo (jana) tumeitwa hapa kwa ajili ya kikao cha robo mwaka (mwaka wa fedha wa 2016 – 2017) ambacho kilitakiwa kufanyika mwezi wa sita, lakini kilishindikana kutokana na mgogoro baina ya mkurugenzi, (Kiomoni Kibamba), madiwani na Meya,” alisema Pambalu.

Pambalu alisema therusi mbili ya madiwani tayari walikwisha saini waraka wa kutokuwa na imani na meya (James Bwire) hivyo kumtaka asiendeshe kikao chochote mpaka kanuni zitakapofuatwa ikiwa na kusubili vikao vya juu vitakapotoa maamuzi.

Baada ya waandishi wa habari kusubiri kwa masaa sita, Mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kibamba, kufuatia kumalizika kikao cha ndani na madiwani wa CCM aliingia ukumbini na kuhairisha kikao hicho huku akidai kikao hicho kimehairisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Meya wa Jiji hilo, James Bwire, amesema kanuni zinazoongoza vikao hivyo zinaonesha kikao hakiwezi kuhairisha na mkurugenzi wala kufunguliwa na na mkurugenzi bali mwenye mamlaka hayo ni meya ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kiundani zaidi, alidai hawezi kuzungumza kwa kuwa kikao hicho hakukifungua.

Tangu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, kuanza kuliongoza Jiji hilo, amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na Meya huyo kwa kile kinachotajwa ni maslahi yao binafsi yanayosababisha mgogoro huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!