Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM Mwanza: Kauli ya Ndugai ni ya kihuni
Habari za Siasa

CCM Mwanza: Kauli ya Ndugai ni ya kihuni

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dk. Anthony Diallo
Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, kimesema kauli iliyotolewa na Spika wa Bunge, Spika Job Ndugai, ya kuwa kuna siku nchi itapigwa mnada kutokana na kuelemewa na madeni, ni kauli ya kihuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 31 Desemba 2021 na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dk. Anthony Diallo, akimjibu Spika Ndugai, kufuatia kauli yake hiyo aliyoitoa tarehe 27 Desemba mwaka huu, jijini Dodoma.

“Mtu wa namna hi anayesema hivyo ni vizuri tu kumuombea kwa sababu nikiwaulizia ninyi pamoja na uzoefu wenu wa kazi mlisikia taifa gani limepigwa mnada ? Kwa sababu, kwanza ni terminology ya kihuni, sio terminology ambayo unaposema nchi inapigwa mnada haijawahi kutokea,” amesema Dk. Diallo.

Mwenyekiti huyo wa CCM mkoani Mwanza, amesema Spika Ndugai alipaswa kutoa mawazo yake katika mamlaka husika, badala ya kutoa hadharani.

“Kwenye hili mtu kama ana mawazo tofauti basi anatakiwa kupitisha mawazo yake kwenye vyombo vinavyosimamia kichama na Serikali, sababu Serikali iko kamili ina vyombo vyote vinavyohusika na kama kuna tatizo la uelewa watu wengi wana uwelewa,” amesema Diallo.

Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM

Kauli hiyo ya Dk. Diallo ni muendelezo wa viongozi wa CCM wa mikoa, kupinga msimamo wa Spika Ndugai, wa kukosoa hatua ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kukopa kiasi cha Sh. 1.3 trilioni, kutoka kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Kwa ajili kukabiliana na athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), ikiwemo kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya, elimu na miundombinu.

Miongoni mwa mikoa iliyotoa tamko la kumpinga Spika Ndugai na kumuunga mkono Rais Samia, ni Dar es Salaam na Singida.

Diallo amesema, fedha hizo zilizokopwa na Serikali ya Rais, zinalenga kumaliza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, iliyoanzishwa na awamu zilizopita.

Job Ndugai

Pia, Diallo amesema, fedha hizo zitasaidia kukabiliana na janga la UVIKO-19, kwani zitatumika katika utekelezaji wa miradi katika sekta ya afya na elimu, inayosaidia kudhibiti kasi ya usambaaji wake.

“Wakati huu kuna ugonjwa, wanafunzi wangekaa kama wanavyokaa 100 kwa darasa moja, ingesumbua zaidi, huu ugonjwa unahitaji maji tiririka yasingetoka kwenye madimbwi lazima miradi ya maji ingeangaliwa,” amesema Dk. Diallo na kuongeza:

“ Kuna miradi ya barabara vijini, vituo vya afya, hospitali zinakuwa na vifaa vya kisasasa kuliko ilivyokuwa nyuma. vifaa tiba vitaongezwa kuhudumia wagonjwa wa UVIKO-19.”

1 Comment

  • Asante ccm mwanza mnastahili pongezi sana wale wasaliti wa ccm watambue kwamba wamepanda mbegu hewa sasa wajiandae kuvuna kimbuga mmoja wapo aliyejitambusha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!