Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM: Msajili wa Vyama vya Siasa adhibitiwe
Habari za SiasaTangulizi

CCM: Msajili wa Vyama vya Siasa adhibitiwe

Rais John Magufuli akiongoza Kamati Kuu ya CCM
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) jana kimepitia na kudadavua Muswada wa Sheria wa Vyama vya Siasa na kubaini udhaifu wake. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Katika mkutano huo, kimetaka Msajili wa Vyama vya Siasa adhibitiwe baada ya mswada huo kutaka kumpa mamlaka yaliyopindukia dhidi ya vyama vya siasa nchini.

Wakati CCM wakipinga baadhi ya vipengele kwenye muswada huo, Mahakama Kuu Tanzania tayari imetupilia mbali shauri la kupinga muswada huo lililowasilishwa na wanachama watatu wa upinzani.

Wanachama waliofungua shauri kupinga muswada huo kwa madai ya kukiuka Katiba ya Nchi ni Zitto Kabwe, Salumu Biman na Joran Bashange.

Zitto ambaye ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Biman Mkuregenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi (CUF) na Bashange Naibu Katibu (CUF) Bara.

Viongozi hao waliowakilisha vyama 10 vya upinzani, walifungua shauri hilo kupinga muswada wa sheria hiyo usijadiliwe bungeni kupitia jopo la mawakili wao walioongozwa na Mpoki Mpare.

Baadhi ya wanachama, wajumbe na viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano huo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, walionesha mashaka kutokana na nguvu kubwa anayotaka kupewa msajili.

Leah Mbeke, Katibu wa Vijana Wilaya ya Ubungo ameshangazwa na kifungu cha 8E kinachoeleza kuwa, vikundi vya ulinzi vya vyama vya siasa kufutwa.

Leah amesema kuwa, haoni sababu ya kuwepo kwa kipengele hicho kwa kuwa, haki ya wanachama kulinda viongozi wao ipo wazi.

Alihoji “kwa hiyo hatutakiwi kulinda viongozi wetu?”, alikwenda mbali na kumtolea mfano Humphrey Polepole kwamba, anawezaje kukosa haki ya kumlinda?

Leah alisema, vyama vya siasa vina mali pamoja na viongozi hivyo kuna kila sababu kuwepo kwa vikundi vya ulinzi kwa ajili ya usalama wa viongozi pamoja na mali za chama.

Mjumbe wa mkutano huo ambaye pia ni mwanasheria Leonard Manyama alishangazwa na kipengele kinachotaka vyama vya siasa vinapoendesha mafunzo kwa wanachama wake, vipeleke taarifa kwa msajili.

“Hivi chama kinapotaka kutoa mafunzo kwa wanachama wake kinapaswa kutoa taarifa kwa msajili?” amehoji Manyama huku akitoa pendekezo la kuangaliwa upya kwa kipengele hicho.

Miongoni mwa vipengele vilivyopendekezwa kwenye muswada huo ni msajili kufanya kazi ya kutoa mafunzo ya uraia kwa wanachama wa vyama vya siasa. Ni kipengele 4(F) cha muswada wa sheria ya vyama vya siasa.

Raymond Mwangwala, Katibu wa UVCCM amekinzana na pendekezo hilo akitaka kazi hiyo ifanywe na vyama vya siasa vyenyewe badala ya kufanywa na msajili.

Polepele amependekeza kazi ya kutoa elimu kwa wanachama isifanywe na msajili kama ilivyopendendekezwa na badala yake ifanywe na vyama vya siasa vyenyewe.

Pamoja na kutaka marekebisho ya vipengele hivyo, WanaCCM hao wameunga mkono baadhi ya mapendekezo ikiwa ni pamoja na msajili kusimamia na kufuatilia chaguzi za ndani za vyama hivyo, msajili kuwa na orodha ya wajumbe wa vikao pamoja na pia kusimamia ruzuku za vyama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!