May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM kuwahoji Askofu Gwajima, Polepole na Silaa

Askofu Josephat Gwajima

Spread the love

 

WABUNGE watatu wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), watawekwa ‘kitimoto’ na Kamati ya Maadili ya chama hicho, juu ya tumuma mbalimbali zinazowakabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wabunge hao ni Askofu Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Ukonga) na Humphrey Polepole (Kuteuliwa) ambao watafika mbele ya kamati hiyo leo Ijumaa, tarehe 3 Septemba 2021, Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dodoma.

Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na Silaa, watafika mbele ya kamati wakiwa wanaendelea kutumikia adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge, huu unaoendelea na Novemba 2021 na watarejea tena bungeni Januari 2022.

Humphrey Polepole

Ni baada ya kukutwa na hatia na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyowahoji Askofu Gwajima na Silaa iliyowahoji kuhusu tuhuma mbalimbali ikiwemo za kusema uongo.
Baada ya kupewa adhabu hiyo, kamati ilishauri mamlaka zingine ikiwemo chama chao- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwachukulia hatua.

Katibu wa Wabunge wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa Mlalo Mkoa wa Pwani, Rashid Shangazi amesema, “tumewaita ili na sisi tuweze kuwahoji na kuwasikiliza katika kikao cha maadili ya chama.”

“Lakini pamoja na waheshimiwa hao Askofu Gwajima na Silaa, tumemwita Polepole naye atakuwa sehemu ya kamati hiyo ya maadili kwa ajili ya mahojiano mbalimbali,” amesema.

error: Content is protected !!