December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM kuwafyeka ‘wateule wa Rais’ walioanza kampeni mapema

Rais John Magufuli akiongoza Kamati Kuu ya CCM

Spread the love

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania amewatangazia kiama, watumishi wa umma, wakiwemo wateule wa Rais John Magufuli walioanza kampeni mapema za uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020 kwamba  hawatopitishwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam leo Ijumaa tarehe 22 Mei, 2020, Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho amesema muda wa kuanza kampeni haujafika.

Polepole amesema, viongozi walioanza kampeni mapema, “hawatapewa dhamama kwenye Chama cha Mapinduzi, na hii inakwenda sambamba na baadhi ya watumishi kwenye Serikali ambao wanafanya vurumani kwenye majimbo.”

“Ukipewa kazi kwenye Serikali na Rais, hebu tenda hiyo kazi hadi ikamilike na tuone kweli hii imetokea vizuri hafu Rais atajua namna alikupa hii hafu akupe nyingine,” amesema.

Polepole amesema, “lakini wewe umepewa kazi moja, hujaimalisha unakwenda kuvuruga na hasa majimbo ya CCM.”

“Wako watu wanasema wametumwa na viongozi wa kitaifa, waongo, hakuna mtu aliyetumwa na wakuu wa chama, mwenyekiti, makamu wake wawili, katibu mkuu mimi hapa msemaji kwa niaba ya chama na viongozi wote wa kitaifa,” amesema.

Polepole amesema ndani ya chama hicho, kila mwanachama ana haki sawa, “pale tunapotafuta uongozi binadamu wote ni sawa. Tutakapopuliza kipenga cha kuomba dhamana ya uongozi, ndipo hapo watu watapaswa kuomba.”

“Kinyume na hapo, wote wanaojipitisha pitisha majimboni kiamana ndani ya CCM kinawasubiri,” amesisitiza.

Katika mkutano huo, Polepole amesema, mchakato wa kuandika Ilani ya uchaguzi mwaka 2020/2025 na sera imekamilika na, “ilani ya CCM ni nzuri, nzuri mno, ina fursa kubwa ambazo hazijapata kutokea.”

Kutokana na maambukizi ya virusi vya corona kupungua nchini, Polepole amesema chama hicho kimeruhusu kufanyika kwa shughuli zote za chama ikiwamo maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 2020.

error: Content is protected !!