Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM kumchomoa ‘mtu wao’ Dk. Mashinji leo?
Habari za Siasa

CCM kumchomoa ‘mtu wao’ Dk. Mashinji leo?

Vicent Mashini, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema (kushoto) akiwa na Humphrey Polepole, Katibu wa Itibaki na Uenezi wa CCM muda mchache baada ya kumpokea mwanachama huyo mpya
Spread the love

MAISHA ya kutengwa, kuzomewa na hata kupuuzwa anayopita Dk. Vicent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yanapata faraja kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Humprey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema, wanaelekea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukamilisha utaratibu za kulipa faini ili kumtoa Dk. Mashinji.

Dk. Mashinji ni miongoni pamoja na viongozi nane wa Chadema, wamehukumiwa kulipa faini bama kwenda jela miezi mitano baada ya kukutwa na makosa katika mashitaka 12 kati ya 13 walisyoshtakiwa. Dk. Mashinji pekee anatakiwa kulipa faini ya Tsh. 35 Mil.

Awali, CCM iliendesha zoezi la kuhakikisha Dk. Mashinji anarudi uaraiani leo tarehe 11 Machi 2020.

“Zipo harakati zilizoanza kabla ya hukumu jana, tuliamini Dk. Mashinji na wenzake wasingeweza kuachwa tu kutokana na tuhuma zile.

“Sio kama chama kilikuwa usingizini, kilijua na ndio maana taratibu za kupata fedha zilishika kasi muda mfupi baada ya kujua mahakama inahitaji nini ili awe free (huru), nadhani sasa ni suala la utaratibu tuna si pesa tena,” amezungumza ofisa wa chama hicho kutoka ofisi ndogo ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Jana usiku, Polepole aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter, kwamba anashukuru CCM Mkoa wa Dar es Salaam na kamati ya siasa kutokana na kushughulikia suala la Dk. Mashinji.

“Asante CCM Mkoa wa DSM, Mwenyekiti na Kamati ya Siasa kwa kujitoa kwenu kwa haraka ili kesho tukamnusuru Mwanachama wa CCM Vicent Mashinji.

“Mtakumbuka kuongoka kwa Mashinji kumetupa picha nzuri ya wasiotutakia mema na mipango yao mingi yenye nia ovu,” aliandika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!