July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM inanyonya wafanyakazi-Kafulila

Maandamano ya walimu katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi iliyofanyika jijini Mwanza

Spread the love

WAKATI wafanyakazi duniani wakisheherekea siku kuu yao, David Kafulila-Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), amesema wafanyakazi wa Tanzania wanaumizwa sana katika kodi kuliko wafanyakazi wa nchi zote za Afrika Mashariki. Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).

Amesema kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM), asili yake ni harakati za wafanyakazi na wakulima wadogo na ndio tafsiri ya alama ya jembe na nyundo kwenye bendera yake.

“Hivyo, ni aibu chama kilichoasisiwa na wafanyakazi, leo kinaongoza kunyonya wafanyakazi kwa kodi kubwa kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki.

Katika ujumbe wake kwa wafanyakazi, Kafulila amesema, wastani wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni asilimi 12, Uganda 11, Kenya 6.8, Burundi 10.3 na Rwanda 5.6 kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya global tax comparison 2014.

Kafulila amesema, wastani wa kodi ya mfanyakazi duniani kwa mujibu wa ripoti hiyo ni asilimia 16.2. Kwamba, kwa takwimu hizi sio tu wastani wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni kubwa kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki bali ni zaidi ya wastani wa kodi ya mfanyakazi duniani.

“Nashauri wafanyakazi waombe CCM iondoe nembo ya nyundo kwenye bendera yake kwani ni kejeli kwao. CCM kwa sasa ipo kwa maslahi ya wafanyabiashara wakubwa wasio waaminifu. Hao ndio wanafaidi uchumi kwa misamaha ya kodi na ukwepaji mkubwa wa kodi.

“Ni maoni yangu kwamba, kodi ya mshahara inapaswa kushuka kwa asilimia 50. Itoke asilimia 12 mpaka asilimia 9 wastani kwa kuanzia. Kwa mujibu wa taarifa za TRA mwaka jana, tukishusha kodi hiyo kutoka wastani wa asilimia 12-9 tutapoteza mapato kiasi cha Sh.704 bilioni,” anasema. 

Kwa mujibu wa Kafulila, ni maoni yake kwamba, mapato hayo yanaweza kufidiwa kwa kutekeleza sheria ya kodi ya majengo ambayo mpaka sasa utekelezaji wake ni asilimia 3 ambapo inakusanya Sh. 25 bilioni.

“Hii maana yake ni kwamba, tukiteleleza kwa asilimia 100, tutakusanya zaidi ya Sh. 800 bilioni,” anasema.

error: Content is protected !!