Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge wa upinzani amtabiria anguko Rais Magufuli 
Habari za Siasa

Mbunge wa upinzani amtabiria anguko Rais Magufuli 

Rais John Magufuli akiongoza Kamati Kuu ya CCM
Spread the love

JOHN Heche, mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Tarime Vijijini, amedai kuwa hatua ya Rais John Magufuli, kuzuia mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, imezidi kumuongezea maadui ndani ya nje ya chama chake. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Amesema, “hatua hii, imeshindwa kumsaidia mbele ya wananchi. Badala yake, kitendo hicho, kimemchafua mbele ya uso wa dunia na kimemuongezea chuki kwa wananchi.”

Anaongeza, “hatua yake ya kuzuia mikutano ya hadhara na vyama kufanya kazi zake za kisiasa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, imezidi kuchochea wananchi kukichukia Chama Cha Mapinduzi (CCM), na hivyo kurahisisha kazi yetu ya kukiondoa madarakani katika uchaguzi ujao.”

Heche alitoa kauli hiyo, katika mahojiano yake na MwanHALISI Online, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya tarehe 19 Aprili 2019.

Aidha, mwanasiasa huyo amesema, mtindo unaotumiwa kwa sasa na serikali ya Rais Magufuli wa kuwakamata viongozi wa upinzani, kuwaweka ndani, kuwafungulia mashitaka na hata vitishoni, “ni dalili ya ujio wa anguko kwa chama hicho.”

Amesema, CCM haina tena uwezo wa kushindana kisiasa. Ndio maana inatumia nguvu kuzima hoja za wapinzani.

Kwa mujibu wa Heche, kitendo cha chama hicho kuwafungulia kesi viongozi wa upinzani, wabunge na wafuasi wao, katika mahakama mbalimbali nchini, kinaashiria kuwa CCM kimekumbwa na mkwamo wa kisiasa na hivyo inatafuta mbinu za kuziba midomo wapinzani wake.

“CCM wameshindwa kujibu hoja zetu. Watu tuliopaswa kushindana nao kisiasa wamepoteza uwezo wa kushindana; badala yake wameamua kutumia dola kutunyamazisha,” ameeleza.

https://www.youtube.com/watch?v=STkcmaNMwV0

Amesema, “wanatuzuia kufanya mikutano ya kisiasa. Wanakwenda kutishia vijana wetu wa vyuo vikuu kwa kuwambia wasipojiunga na chama chao, basi hawatapata kazi serikalini. Yote haya ni dalili za mwisho za kuanguka kwa serikali ya Rais Magufuli.

“Mifano iko duniani, mwanzo watu wanashindana, mkiwashinda hoja wataingiza dola, watawakamata, wataweka magereza baada ya muda mrefu mwisho huwa wanaanguka.”

Heche anasema, wananchi hawawezi kukubali kupiga magoti kwenye mabavu.  Hawawezi kuwapigia magoti wadhalimu. Kuna siku wataamka na kupambania taifa lao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!