January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM Dodoma: Wanaopanga kugombea urais 2025 ni wachawi

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk. Damas Mkasa

Spread the love

 

JUMUIYA ya Wazazi CCM – Mkoa wa Dodoma imelaani ‘genge’ la watu wachache ambao wamepanga njama za kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kudai kuwa watu hao ni sawa na wachawi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja imepita baada ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, kubainisha wazi kuwa ndani ya chama hicho kuna kundi lenye homa ya uchaguzi mkuu 2025 ambalo linalenga kumkwamisha katika juhudi za kuwaletea maendeleo Watanzania.

Aidha, akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 5 Januari, 2022 na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk. Damas Mkasa pamoja na mambo mengine pia amempongeza na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na maono makubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Dk. Mkasa amesema kati ya mashati ya kijani ambayo yatapambana kuhakikisha wanamuunga mkono Mwenyekiti CCM taifa na rais wa sasa ni pamoja na jumuiya ya wazazi mkoa wa Dodoma ukiondoa wachache ambao wamechanganyikiwa kwa kuwa na uchu wa madaraka.

“Dodoma ndipo ilipo ngome ya chama hivyo Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dodoma haiwezi kukubaliana na watu wachache ambao hawajitambui, wapuuzi kwa kutokutambua kazi kubwa zinazofanywa na Rais Samia.

Amesema kuwa wanaCCM ambao wanauchu wa madaraka, wanafiki na wazandiki waache mara moja kwani chama kina misingi yake ambayo inajali maadili.

“Nataka kuwaambia ndugu zangu wana CCM tuache unafiki, uzandiki, majungu na ninaweza kusema watu wa aina hiyo ni sawa na wachawi ndani ya chama.

“Tuliapa kwa kusema kuwa nitasema kweli kwangu fitina ni mwiko, kiongozi yoyote anatoka kwa Mungu, leo hii makundi ya watu wasiokuwa na akili ndani ya chama wanaopanga mbinu za kumhujumu rais wanapata nguvu wapi kama siyo kuwa na roho mbaya na unafiki?

“Tumekuwa na marais kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya sasa mbona hatujawahi kuwa na makundi ya kuanza kujinadi kabla ya wakati na kuona kiongozi aliyepo madarakani hafai sasa huu ushetani unatoka wapi? amehoji Dk. Mkasa.

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai

Amesema jumuiya itaendelea kumuunga mkono kwani kwa muda mfupi ameweza kufanya mambo mengi ya kimaendeleo hususani miradi iliyotokana na fedha za mkopo wa mashariti nafuu ya uviko-19.

Tamko hilo la Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dodoma linatokana na hotuba ya Rais Samia kwa kukemea makundi ndani ya chama chake na kuwashangaa wanaobeza mikopo na tozo.

Hata hivyo, chimbuko la yote ni kauli ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ambaye Desemba 27 alitoa kauli ya kumbeza Rais Samia kuwa serikali yake inakopa sana na kuna siku nchi itapigwa Manda.

Hata hivyo Spika ndugai aliibuka na kusema kuwa siyo maneno yake bali yametengenezwa na kuomba msamaha.

error: Content is protected !!