June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM chamuogopa Lowassa

Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba akizongwa na waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemuogopa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kwa kuogopa kujitokeza hadhara kujibu tuhuma kuwa ni cha majungu, fitna na mizengwe katika hotuba yake baada kutangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). MwanaHALISI Online limeambiwa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Chanzo cha habari kutoka CCM (jina linahifadhiwa) kinasema kwamba kabla ya leo kulikuwa na vikao vilivyoketi usiku kucha kilicholenga “kuendelea kujibizana na Lowassa” ili asifanikiwe katika azma yake ya kuendelea na safari yake ya matumaini ya urais na kuking’oa CCM madarakani kupitia Ukawa.

“Katika kutekeleza lengo hilo, jana mchana CCM ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba leo saa 7 mchana Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa chama hicho angezungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CCM yaliyopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam,” kimesema chanzo cha habari.

Aidha, jana mchana MwanaHALISI Online liilipata taarifa za mwaliko huo ambapo leo lilihudhuria.

Katika hali iliyozua taharuki kwa waandishi wa habari, mkutano ulifanyika katika Hoteli ya Peacok huku Nape kutokuwepo huku Katibu Mwenezi CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba akijitokeza na kusema yeye ndiye mzungumzaji wakati mkutano huo angeweza kuufanyia ofisini kwake kama lengo kweli lilikuwa ni hilo.

Katika hali iliyoendelea kuzua mshangao kwa waandishi wa habari, Juma alianza kuzungumza kwa kuwapongeza wanachama wa CCM kwa kushiriki katika uchaguzi uliofanikisha kumpata mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufuli huku akiitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhakikisha kila kila mwananchi anajiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga kura.

Alipoulizwa wako wapi viongozi wa kitaifa akiwemo Nape kama ambavyo waandishi walipokea taarifa za mkutano huo amesema kwa ufupi, “Hata mimi ni kiongozi wa kitaifa sijui mnamtaka nani.”

Aidha, Juma aliulizwa nini maoni ya CCM Kutokana na Lowassa kuondoka ndani ya Chama hicho hasa ukizingatia ana wafuasi wengi ambao wanaweza kumfuata Chadema amesema, “..Lowassa aliingia CCM kwa ridhaa yake. Hakuna mtu aliyeshituka. Na ametoka CCM kwa ridhaa yake. Tunao viongozi wakubwa bado wapo.

Utata uliibuka zaidi baada ya ujumbe unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ukiwa na kichwa cha habari “Taarifa kwa wanachama wa CCM kuhusu mchakato kupata mgombea urais wa CCM”. Taarifa hiyo ilisheheni tuhuma dhidi ya Lowassa ambazo zilipelekea jina lake kuenguliwa katika hatua za awali kumpitisha mgombea urais wa chama hicho.

MwanaHALISIOnline lilimtafuta Nape ili aweze kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hiyo mpaka tunaiweka habari hii mtandaoni hakupatika.

error: Content is protected !!