August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM, Chadema wamng’oa mwenyeviti Singida

Wanaijiji cha Unyianga, tarafa ya Unyakumi, Singida wakiwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kijiji hicho

Spread the love

WANANCHI wa kijiji cha Unyianga, Manispaa ya Singida wamemvua madaraka Sombi Goda Mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji kwa tuhuma za kutosoma taarifa ya mapato na matumizi ya Kijiji hicho kwa kipindi cha miaka mitatu, anaandika Mwandishi Wetu.

Uamuzi huo umetolewa katika mkutano mkuu wa kijiji na wanakijiji wote bila kujali itikadi za vyama vyao wakidai kuwa wamechoshwa na vitendo vya viongozi hao ambapo katika viwanja vya mikutano vya ofisi za kijiji hicho walipiga kura na kumkataa mwenyekiti na wajumbe wake wote.

Wajumbe wa serikali ya kijiji hicho walioondolewa madarakani kwa mujibu wa Halima Kalungwani Ofisa mtendaji wa kijijini Ramadhani Nyangu, Gidion Kisuke, Shabani Nyangu, Issah Mussa Mpaki, Joseph Makhata Timo, Khadija Hassani, Amina R. Sunja na Ayubu S. Mpanya.

Wengine ni Joseph S. Ngoy, Edward Nkindi, Hamisi Mkanga, Omari Laghaa, Halima Mkanga, Fatuma Msengi, Joseph Makhata, Ramadhani Kilume, Ernesti Kikhando, Obedi Ngoy, Abdallah Goda, Ramadhani Mbaya, Issa Maliwa, Helena Sakali Makusa, Elia Ntandu, Khadija Hassani na Shabani Nyangu.

Mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya watu mia tatu, akiwemo Geofrey Mdama diwani wa kata ya Unyianga ambapo licha ya mwenyekiti na wajumbe wake kuomba msamaha kwa kosa la kutosoma mapato na matumizi kwa miaka mitatu lakini wananchi walichachamaa na kuwang’oa.

“Tumechoka sana kuibiwa na kudhulumiwa haki zetu kwani kwanza tulikuwa tukiibiwa wakati kata ilikuwa mbali huko Mwankoko na hata sasa kata ipo miguuni katika Kijiji chetu cha Unyianga tuendelee kuibiwa tu, haiwezekani,” walisikika wakisema baadhi ya wananchi hao.

Ofisa Mtendaji wa kata ya Unyianga, Habiba Juma aliwahakikisha wananchi hao kwamba walichokuwa wakidai ni haki yao ikiwemo kusomewa taarifa ya mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu na kwamba kuanzia mwezi wa kumi hadi sasa hakuna mapato yeyote yaliyokusanywa kwenye vibanda vilivyopo Kijijini hapa.

Naye Geofrey Mdama diwani wa kata ya Unyianga, aliweka bayana kuwa baada ya wananchi walioanza kususia mkutano huo kurejea tena kwenye viwanja hivyo,alitumia fursa hiyo kuwataka watoe maamuzi wanayodhani yataleta tija kwa upande wao na Kijiji hicho kwa ujumla na ndipo walipopendekeza kura ipigwe kupata muafaka wa suala hilo.

error: Content is protected !!