Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila
Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amepiga marufuku tabia za wazazi na walezi nchini kuwatumia watoto wakike katika shughuli za kimila ikiwemo kuwacheza ngoma na kuwaozesha mapema kwa kuwageuza chombo cha kujipatia mali na mitaji bali wawasomeshe ili waweze kuwasaidia zaidi baadae. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Chongolo alisema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM shina namba mbili lililopo kwenye Kijiji Cha Kiroka Wilayani Morogoro ambapo alisema kumsomesha mtoto wa kike ni mtaji mkubwa sana kwa sababu anapofanikiwa hawezi kuwaacha wazazi wake wakihangaika tofauti na mtoto wa kiume ambaye huelemea kwa mke aliyemuoa.

“Katika wilaya hii hatupatii kipaumbele watoto wa kike katika suala la elimu bali hukimbilia kuwacheza ngoma na kuwaozesha kwa lengo la kupata mali, tutambue kuwa mtoto wa kike sio chombo cha kupatia fedha, wala mali, wala utajiri kwa kumuozesha bali ukimsomesha itamsaidia kupata kazi nzuri, na mshahara mzuri utakaomuwezesha kuwalea wazazi wake hata atakapoolewa” alisema.

“Wazee acheni Mambo ya kupokea mahali na kuwekea ahadi watu juu ya kuwaoza watoto wenu, muendelee kuwalea kimaadili na elimu ili muwafanye kuwa watoto wanaoweza kuajiri wengine na sio wao kuajiriwa kuwa watumishi kwenye nyumba za watu” alisema Chongolo.

Alisema  tabia hiyo ya wazazi isipodhibitiwa itaendelea kuwa kigingi kwa watoto wengi wakike wilayani Morogoro kutoonja radha ya elimu.

Hata hivyo aliwataka wazazi kujenga tabia ya kujua mienendo ya vijana wao na kufuatilia kazi wanazofanya hasa wanapopata mafanikio wajue wamepataje ili kuepukana na kupata watoto wenye tabia za udokozi na wizi.

“Ukimuona mwanao mwizi au wanamwambia mwizi maana yake umeacha malezi, msiwashangilie watoto wanapokuja na mafanikio, jueni mafanikio hayo yamekujaje, sababu mtoto ni bodaboda, anapata hela ya kipande ya kumpa bosi na ya kula mwenyewe, baada ya miezi miwili anakuja na boda yake anakwambia anampa mtu amuendeshee, ulizeni wamepata wapi ” alisema Chongolo.

Hata hivyo alikemea tabia za jamii kuzingatia mila potofu kwa wagonjwa wakiwemo kinamama wajawazito ambao huwapa dawa na kuacha kuwakimbiza hospitali na kuhatarisha uhai wao.

Aidha aliwatoa hofu wakazi wa vijiji vya eneo hilo kuwa barabara ya Bigwa – Kisaki itajengwa kwa kiwango cha rami na kurahisisha usafiri na usafirishaji bidhaa Wilayani humo ambapo aliagiza TANROADS kuhakikisha wanaweka taa za barabarani kilometa 10 kila panapokuwa na mji.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba alisema ujenzi wa barabara ya Bigwa – Mvuha- Kisaki – Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa kiwango cha rami unatarajia kuanza mwezi Juni mwaka huu.

Mhandisi Kyamba alisema ujenzi wa barabara hiyo utahusisha ujenzi wa madaraja yote ikiwemo la mto Ruvu na Mvuha.

Naye Meneja wa Wakala wa usambazaji nishati ya umeme (REA) Taifa Mhandisi Romanus Lwena alisema kwa Sasa wapo katika hatua ya kukamilisha kuweka umeme kwenye vitongoji vyote nchini huku wakiwa tayari wameshaweka umeme kwenye vijiji vyote 12,245 vya Tanzania.

Mhandisi Lwena alisema Tanzania ina jumla ya vitongoji 64 ambapo 32 kati ya hivyo tayari walishaweka umeme na Sasa wanamalizia vijiji Vilivyobaki.

Awali Katibu wa siasa na uenezi CCM NEC Taifa Sophia Mjema aliwataka wanachama wa CCM kuendelea kukiimarisha Chama kwa kutaja na kusema mema yote ambayo yamefanywa ili kuifanya jamii kutokuwa na maswali .

Mjema alisema maendeleo yote yaliyotendeka na yanayotendeka yametokana na mafanikio ya Serikali ya CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!