Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu CBE yazindua klabu ya ujasiriamali sekondari ya Temeke Wailes
ElimuHabari

CBE yazindua klabu ya ujasiriamali sekondari ya Temeke Wailes

Spread the love
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimezindua klabu ya ujasiriamali kwa shule ya sekondari Temeke Wailes iliyoko Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Uzinduzi wa klabu hiyo ulifanyika jana Ijumaa kwenye shule hiyo

Chuo hicho kimesema vilabu hivyo vinalenga kuwawezesha wanafunzi kukua wakifahamu masuala mbalimbali ya biashara tangu utotoni ili waweze kuwa wajasiriamali siku za mbele.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Shahada za Juu, Tafiti na Ushauri wa chuo hicho, Dk. Tumaini Ubadius, alisema wanalenga kuzifikia shule zote za Dar es Salaam.

Dk. Tumaini alisema chuo hicho kimeona ni muhimu wanafunzi wakaanza kufundishwa kuhusu ujasiriamali wakiwa wadogo ili wanapohitimu elimu ya juu wawe na uelewa mpana kuhusu masuala ya biashara.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Wailes iliyoko Temeke jijini Dar es Salam wakionyesha utaalamu waoa wa kutengeneza sabuni shuleni hapo mbele ya viongozi kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), walipoenda shuleni hapo kufungua klabau ya ujasiriamali.

Alisema kupitia mpango huo, chuo kitakuwa kikipeleka walimu wake kila siku ya Alhamisi kwaajili ya kufundisha wanafunzi wanaosomea mchepuo wa biashara masuala ya ujasiriamali.

“Tunataka kupunguza tatizo la watu kutafuta ajira ili wanapomaliza masomo yao waweze kujiajiri na tunachofanya ni kukuza vipaji na ubunifu walionao tangu wakiwa wadogo,” alisema

“Tumeona tuanze kuwajengea uelewa kuanzia huku chini ili kijana anapokuwa aweze kuwa na ufahamu mazingira yanayomzunguka na changamoto zinazomzunguka kuwa fursa kwake kwa kusaidia jamii na kujiingizia kipato,” alisema

Alisema wamepanga kutembelea shule zote za Dar es Salaam na kuanzisha klabu kama hizo lakini wataenda kwenye mikoa ambayo CBE ina kampasi zake kama Mbeya, Mwanza, Dodoma na Zanzibar.

Mkuu wa shule hiyo, Catherine Mdachi aliushukuru uongozi wa CBE kwa kuichagua shule hiyo kuwa miongoni mwa shule za mwanzo kuwa na klabu hiyo.

“Kuna mkuu wa shule moja alinipigia simu kuniambia hivi kwanini hao CBE wameamua kuja huko na kuja huko kwenu nikawaambia ni habati yetu,” alisema

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutujengea madarasa ili watoto wetu wapate sehemu ya kusoma, Huku Temeke hatujui nyota ya kijani tuna watoto wengi lakini tunamshukuru mama ametujengea madarasa mengi,”

Alisema uamuzi huo wa CBE umekuja wakati muafaka kwasababu kuna tatizo kubwa la ajira kwa hiyo kuwafundisha wanafunzi ujasiriamali kutawasaidia kujiajiri kwa kuanzisha biashara zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

error: Content is protected !!