Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu CBE yawashukuru waliochangia harambee, yakusanya shilingi milioni 56
ElimuHabari

CBE yawashukuru waliochangia harambee, yakusanya shilingi milioni 56

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee ya kutafuta fedha za kujenga mabweni ya wasichana kwenye kampasi ya chuo hicho mkoani Mbeya, iliyofanyika Jumamosi iliyopita. Kulia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali chuoni hapo, Dk Shima Banele na kushoto ni Naibu Mkuu wa chuo Mipango na Fedha, Dk. Emmanuel Munishi
Spread the love

 

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimefanikiwa kukusanya shilingi milioni 56 kwaajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana kwenye kampasi yake ya Mbeya na imewaomba wananchi kuendelea kuchangia.

Ombi hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwitikio wa harambee hiyo.

“Kwa niaba ya mlezi wa Kampasi ya CBE Mbeya, Dk. Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni Spika wa Bunge naomba niwashukuru wadau wote waliofika kwenye hafla za kilele cha harambee ya ujenzi wa hostel za watoto wa kike siku ya Jumamosi tarehe 24/09/2022 iliyofanyika katika Ukumbi wa hotel ya Eden Highlands Mbeya. Tunawashukuru watu wote waliohudhuria na kuchangia katika kilele cha changizo la hosteli za wanafunzi wa kike, CBE kampasi ya Mbeya,” alisema Mjema.

Aidha, alimshukuru na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa kuendeshea shughuli ya harambee hiyo  ya changizo na kuweza kuchangisha kiasi hicho cha fedha.

Alimshukuru pia Dk Tulia Ackson ambaye pia ni mlezi wa Kampasi CBE Mbeya kwa kuanzishia na kusimamia harambee hiyo tangu alipoizindua yeye mwenyewe Mwaka jana.

Alisema harambee hiyo inalenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwaajili ya ujenzi wa hostel za watoto wa kike huku akitoa wito kwa wadau kuendelea kuchangia kwani wanahitaji pesa zaidi kwani bado hawaujafikia malengo waliyojiwekea.

Naibu Mkuu wa chuo Mipango na Fedha, Dk. Emmanuel Munishi akizungumza kuhusu harambee hiyo iliyofanyika mkoani Mbeya Jumamosi iliyopita. Katikati ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema na kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Shahada za awali chuoni hapo, Dk Shima Banele

“Kwa wale watakaoendelea kuguswa tutaendelea kupokea na kutambua michango yao kwa kutoa tuzo katika makusanyiko makubwa ya Chuo chetu. Nawashukuru pia, wabunge ambao wameendelea kutoa michango yao ya hali na mali ni vigumu kuwataja majina yao ila mwisho kabisa wa jambo hili tunaweza kutoa majina ya Taasisi, Makampuni na watu binafsi walioguswa na kampeini ya Changizo hili,” alisema.

Aliwaomba wadau wote wenye mapenzi mema na maendeleo ya nchi yetu walipo ndani na nje kuendelea kuwashika mkono kwa kuchangia chochote ili tuweze kukamilisha harambee hiyo kwa kuendelea kumuunga mkono mlezi wa Kampasi ya CBE, Dk.  Tulia Ackson.

“Aidha niiwaombe wadau wote ambao tumewafikia na ambao watapata ujumbe wetu kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwamba kwa wale wanaoendelea kuguswa na jambo hili tutaendelea kupokea na kutambua michango yao wakati ujenzi wa hosteli unaendelea. Naomba nisisitize kuwa jambo letu la Changizo la Ujenzi wa Hostel za Wanachuo wa kike yenye kauli Mbiu, “Changia zaidi ya harusi, uwe sehemu ya kuleta tabasamu kwa mtoto wa kike,” alisema

Katika hatua nyingine, Profesa Mjema alisema tarehe 08/10/2022 watakuwa na hafla ya ufunguzi rasmi wa majengo na Kampasi ya CBE Mbeya ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa.

Profesa Mjema alisema kwa wachangiaji wakubwa watakaojitokeza na wale ambao tayari watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo.

“Mwishoili siyo kwa umuhimu, tunaendelea kuwakaribisha wale wote ambao hawakuweza kuhudhuria tukio letu la changizo la tarehe 24/09/2022 kuleta michango yao siku ya Ufunguzi wa Kampasi na Majengo ya chuo. Pia, Chuo kitaendelea kutambua wachangiaji katika sherehe mbalimbali ikiwemo Mahafali ya 57 katika kampasi zetu na Katika Ufunguzi wa Kongamano la kimataifa litakalofanyika jijini Dodoma tarehe 15 Novemba, 2022,” alisema.

Alisema kwa wale watakaoguswa na jambo hilo wachangie kupitia NMB BANK akaunti ya chuo hicho -20601100030, AIRTEL  567567 na MPESA – 977992

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!