Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu CBE yatamba kuzalisha wahitimu walio tayari kwa soko la ajira
ElimuHabari

CBE yatamba kuzalisha wahitimu walio tayari kwa soko la ajira

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Edda Tandi Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kozi ambazo zitaanza kufundishwa mwezi tisa Kushoto ni Mhadhiri Mwandamizi wa chuo hicho, Dk. Nasibu Mramba na kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa chuo hicho, Leonidas Tibanga
Spread the love

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimesema mpango wa kuwasaidia wanafunzi wajasiriamali kuendeleza biashara zao au kuatamia mawazo ya biashara zao utakuwa wa manufaa makubwa. Na Mwandishi Wetu

Chuo kimesema lengo la kufanya hivyo ni kutatua tatizo kubwa la ajira lililopo nchini kwa  kuwafanya wahitimu wa chuo hicho waendane na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia katika nyanja za biashara na uchumi

Hayo yalisemwa jana na  Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Edda Tandi Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kozi ambazo zitaanza kufundishwa mwezi  tisa.

Alitaja baadhi ya kozi hizo kuwa ni Astashahada ya Msingi ya Uchumi na Fedha, Astashahada ya Msingi ya Usimamizi wa Usafirishaji, Astashahada ya Msingi ya Ujasiriamali na Ubunifu,  Astashahada ya Msingi ya Uongozi wa Biashara, Usimamizi wa Kumbukumbu na Makavazi, Astashahada ya msingi ya Digital Marketing na Astashahada ya Msingi ya Masoko na Utalii .

“Katika ngazi hii tunampokea mwanafunzi ambaye amemaliza kidato cha nne na kufaulu walau masomo manne. Hapa tunaanza kumpa elimu ya Msingi katika fani husika,” alisema.

Alisema kasi inayoongezeka kila mara ya mabadiliko ya kiteknolojia katika nyanja za biashara na uchumi yamekuwa chachu kwa Chuo kuwaandaa wahitimu wanaoendana na mabadiliko hayo.

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Edda Tandi Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kozi ambazo zitaanza kufundishwa mwezi tisa

“CBE imejielekeza zaidi kusaidia katika kutoa mafunzo kwa wahitimu wenye ujuzi wa biashara kwa uchumi wa Tanzania. Chuo kinatambua kuwa maendeleo ya rasilimali watu wenye ujuzi kwa uwezeshaji wavijana, tija, na ufanisi katika jamii unategemea wakufunzi wenye ujuzi na uzoefu, na ubora wa taasisi za mafunzo,” alisema.

Profesa Tandi alisema Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa miaka 58 sasa kimekuwa kikitoa huduma bora katika jamii kwa kutoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali, kutoa wahitimu wenye ujuzi kulingana na uhitaji wa soko na kutoa mafunzo na kutoa ushauri wa kitaalamu.

Alisema mambo hayo yamejikita kwenye majukumu ya msingi ya Chuo ambayo ni Kutoa Taaluma, Kufanya tafiti na Kutoa Ushauri wa Kitaalamu. Ili kuwafikia wananchi wengi Chuo kimeweka huduma hizi katika Kampasi zetu za Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya,” alisema .

Profesa Tandi alisema ili kutoa mchango kwenye Maendeleo ya Viwanda na Biashara Katika Ukuaji wa Uchumi Endelevu Tanzania, Chuo kimekuwa kinabadili mitaala yake na kuongeza kozi mpya zinazoendana na kuendeleza Uchumi, Biashara na Maendeleo ya viwanda.

Alisema katika kukabiliana na Mfumo wa Elimu ya Juu na Kutoa Wahitimu Wasio na Ajira Tanzania, Chuo cha Elimu ya Biashara kimekuwa kikizidi kuongeza matarajio mengi kwa wahitimu kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika na soko la ajira ikiwa ni pamoja na wahitimu wengi kuweza kujitegemea kwa kujiajiri.

“Chuo kimekuwa kikijitahidi kubadili mitaala, kubuni kozi mpya ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu za kisasa za kufundishia. Pia, Chuo kimeanzisha mafunzo ya Uanagenzi vilevile baadhi ya wanachuo kuwa kwenye Atamizi za biashara.  Mafunzo ya uanagenzi yana msingi wa mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na mahali halisi pa kazi. Hapa mwanachuo hutumia nusu ya muda wake Chuoni na nusu kwa mwajiri ambapo hupata fursa ya kujifunza kwa vitendo mambo ambayo tayari amekwisha jifunza kwa nadhalia,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

error: Content is protected !!